WAZIRI MKUU MPYA AANZA KUTEMA CHECHE ,ACHUSHA RUNGU ZITO HOSPITALI YA RUFAA DODOMA KATIKA ZIARA YA KUSHTUKIZA!

 By Arushadigital -DODOMA 

 

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 15, 2025 amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, na kuziagiza hospitali zote nchini zihakikishe ,wajawazito wanapofika hospitali wahudumiwe kwa haraka, ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.


Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Afya, Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali zote nchini, ziweke vipaumbele vya kuwa na dawa kulingana na mahitaji ya eneo husika. “ Haipendezi mwananchi kufika hospitali na kupatiwa vipimo vyote kisha anaambiwa dawa akanunue kwingine, kama duka binafsi linaweza kupata dawa hizo, inawezekanaje hospitali za serikali hapati? Naagiza Hospitali zote ziwe na dawa.”


Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi nje ya hospitali hiyo, baada ya kutembelea wananchi waliofika hospitalini hapo kupata huduma mbalimbali za kitabibu, ambapo amesisitiza wananchi waendelee kuhudumiwa vizuri kwa kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini vikiwemo vifaa tiba na dawa.


Mheshimiwa Waziri Mkuu pi ameziagiza hospitali zote nchini zihakikishe zinakuwa na vifaa vya usafi binafsi vya dharura, vikiwemo ndoo na beseni katika wodi za wazazi, ili viwasaidie akinamama wasiokuwa na vifaa hivyo. “Ujauzito sio suala la dharura vifaa kama ndoo tunapaswa kuwa navyo katika hospitali zetu za serikali.” 





Ends..


Post a Comment

0 Comments