MWIGULU AAPISHWA ,APONGEZWA NA KUTAHADHALISHWA


Rais Samia Ampongeza na Kumpa Onyo Laini Waziri Mkuu Mpya, Dkt. Mwigulu Nchemba

By Arushadigital-Dodoma 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtakia heri na mafanikio Waziri Mkuu mpya, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, huku akimtaka kuwa makini na vishawishi vya ndugu, jamaa na marafiki na badala yake kutanguliza maslahi ya Watanzania.

Akizungumza leo Ijumaa, Novemba 14, 2025, mara baada ya kumuapisha Dkt. Nchemba katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino, Rais Samia alisisitiza kwamba nafasi hiyo kubwa ya uongozi inahitaji uadilifu, uthubutu na moyo wa kujitoa kwa Taifa.

> “Kwa umri wako mizigo ni mikubwa na vishawishi ni vingi kutoka kwa marafiki, ndugu, jamaa na wengine. Nafasi hii haina rafiki, haina ndugu, haina jamaa — ni nafasi ya kulitumikia Taifa. Nikutakie kila la kheri katika utumishi wako,” alisema Rais Samia.

Asisitiza Utekelezaji wa Ahadi za Uchaguzi

Rais Samia amemtaka Waziri Mkuu mpya kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na ahadi walizotoa kwa wananchi, akibainisha kuwa muda wa kufanya kazi ni mfupi na matarajio ya Watanzania ni makubwa.

Aidha, amemwelekeza kutumia uzoefu wake katika Wizara ya Fedha kuhakikisha fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo zinapatikana na kusimamia vyema atakayeteuliwa kushika wizara hiyo ili kasi ya maendeleo iendelee kupaa.



Ends...

Post a Comment

0 Comments