MKE AJITEKA KWA LENGO LA KUJIPATIA PESA KWA MUME MWANAJESHI MSTAAFU

RIBRIS SAFARI KAMPUNI YA UTALII


By Arushadigital 



JESHI la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza taarifa ya uongo kuhusu kutekwa kwa mwanamke aitwaye Hadija Jimmy, mwenye umri wa miaka 39.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Richard Abwao, ametaja watuhumiwa wengine ni Ashura Swalehe (48) na Vitus Joseph (34), ambao wote wanadaiwa kushirikiana kutengeneza simulizi la utekaji kwa lengo la kujipatia fedha.

Amesema watuhumiwa hao walidai kuwa Hadija alitekwa katika Kijiji cha Vumilia, wilayani Urambo mkoani Tabora na kutaka fedha kutoka kwa mume wa Hadija na walifanikiwa kupokea zaidi ya Sh milioni 1.

Kamanda  Abwao, amesema Watuhumiwa hao inaelezwa kuwa walitengeneza uongo huo ili kujipatia fedha kwa mume wa Khadija Murijo, ambako walijipatia kiasi cha takribani Sh. milioni 1.3 kati ya Sh. milioni 2 walizoamrisha kuzipata kutoka kwa Emmanuel.


“Awali walieleza kuwa Khadija alikuwa ametekwa huko Ulyankulu na katika uchunguzi uliofanyika ulibaini kuwa mtuhumiwa huyu alikuwa ameenda Wilaya ya Urambo, Kijiji cha Vumilia na baada ya uchunguzi inaonekana fedha hizi zote walizitolea kwenye Wilaya ya Kaliua. Uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani,” amesema Kamanda Abwao.

Kwa upande wa Mume wa Khadija, Emmanuel Peter Mchali amesema siku hiyo alipigiwa simu na Mke wake na kumueleza kuwa ametekwa na kupata vitisho kutoka kwa mwanaume mmoja kupitia simu ya mkewe, wakimtaka atoe Milioni mbili ili aweze kuachiwa kwa mkewe, suala ambalo lilimlazimu kukopa fedha ili kwenda kulipa kwa watuhumiwa hao.



Aidha, kwa Upande wa mtuhumiwa mwingine Ashura Swalehe ameeleza namna ambavyo alirubuniwa na wifi yake ili kudanganya na kubeba fedha kwa mumewe akidai kuwa Mume wake ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, amekuwa hamhudumii yeye na mtoto wake licha ya kuwa na kipato kikubwa, suala ambalo limekuwa likimfanya kukosa mahitaji muhimu ya kila siku.

Mke
Mume

Post a Comment

0 Comments