By Arushadigital
Mshereheshaji na mchekeshaji maarufu, Emmanuel Mathias anayejulikana kama MC Pilipili amefariki dunia leo Novemba 16,2025.
Taarifa zinaeleza kuwa, MC Pilipili alisafiri kuelekea jijini Dodoma ambapo jioni ya leo alitarajiwa kwenda kufanya kazi yake ya ushereheshaji jijini humo, lakini akafikwa na mauti
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General, Dodoma, Ernest Ibenzi ambaye amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa MC Pilipili amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amefariki dunia.
Msiba huu mzito umewashtua na kuwagusa wengi, ikiwemo mashabiki, wasanii wenzake na wadau wa tasnia ya burudani ambao wameendelea kuonyesha masikitiko kupitia mitandao ya kijamii.
Chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi rasmi na familia wala madaktari, huku mashabiki, wasanii wenzake na watu wa karibu wakiendelea kutoa salamu za rambirambi mitandaoni.
Endelea kutufatilia kwa taarifa zaidi.







0 Comments