By Arushadigital
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Ndugu Luhaga Mpina amewekewa mapingamizi na Serikali, Chama cha AAFP na Chama cha NRA.
Kwa mujibu wa taarifa ya ACT Wazalendo, Usiku wa tarehe 12 Septemba, 2025 majira ya saa 2:36 za usiku, ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho ilipelekewa barua tatu za pingamizi ya uteuzi dhidi ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Luhaga Joelson Mpina. Mapingamizi hayo matatu yamewekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mgombea Urais wa chama cha AAFP, na Mgombea Urais wa chama cha NRA.
Mapingamizi hayo ni pamoja na: Katika hati (fomu) ya uteuzi wa Mgombea Urais kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, jina la Mpina halikuwamo.
ACT Wazalendo imesema imethibitisha kuwa majina yaliyowasilishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa (Msajili) kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hayakuwa sahihi kupitia kwa Mawakili wake kuwa jina la Mpina halikutolewa na Msajili kwa Tume ya Uchaguzi, jambo ambalo lilikuwa kosa la Msajili na si kosa la Mgombea.
Pingamizi la pili lilitolewa limehusu suala la uraia wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina. ACT imejibu kuwa, ushahidi wa vyeti na vielelezo vya kisheria vimewasilishwa kuthibitisha kuwa Mpina ni Mtanzania kwa kuzaliwa na uraia wake haujawahi kubatilishwa.
Pingamizi lingine limehusu mali na maslahi ya kifedha (assets declaration) ya Mgombea. Hoja hii pia imejibiwa kwa vielelezo na ushahidi sahihi kuonesha kuwa Rais Mteule (Candidate for Presidency) amekidhi masharti yote ya kisheria yanayohusu kutangaza mali na madeni yake kwa mujibu wa sheria.
Aidha, ACT imesema inafurahi kuwajulisha Watanzania wote kuwa majibu ya pingamizi yaliyowasilishwa na Chama cha Mapinduzi CCM na Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali yamejibiwa kwa ukamilifu na uthibitisho wa kisheriana kusisitiza kuwaTume ya Taifa ya Uchaguzi itafanya maamuzi ya haki kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.
0 Comments