VIJANA WALIOMKASHFU RAIS SAMIA WATOZWA DUME NNE ZA NG'OMBE,WANAOSUKA RASTA ,KUVAA MLEGEZO,MPASUO MKALI SHERIA YA FIMBO SABINI INAWAHUSU.

 Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 


WATU zaidi ya 5000  kutoka jamii ya wamasai wamejikusanya kukemea vitendo viovu vinavyofanywa na vijana wa jamii hiyo ambao walijirekodi picha mjongeo na  kutoa maneno machafu ya kumkashifu rais wa Nchi


Aidha Jamii hiyo imemwomba radhi Rais Samia Suluhu Hasan kwa kitendo hicho na kutoa karipio kali kwa vijana wa jamii hiyo wanaojiingiza kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo uvutaji wa bangi ,kusuka rasta pamoja na wanawake wanaovaa nguo zenye kuacha sehemu kubwa ya mwili wazi ,kuwa watachukuliwa hatua kali za kimila kwa kuchapwa fimbo Sabini hadharani.


Vijana wanaotuhumiwa kumkashfu rais

Akiongea kwenye Mkutano Mkubwa wa hadhara uliofanyika leo Agosti 1,2025  katika msitu wa mila uliopo kata ya Eleray jijini Arusha,Kiongozi mkuu wa jamii hiyo (Laigwanani) ,Elikisongo Meijo alisema kitendo kilichofanywa na vijana wao wanne  hakikubaliki ni ukosefu wa maadili  na kuitaka jamii hiyo popote nchini kuzingatia maadili waliofunzwa kipindi cha kwenda jando.


Alisema jamii hiyo imewapa adhabu ya kila mmoja kutoa dume moja la Ng'ombe ambao wamechinjwa na kuliwa leo katika mkutano huo .


"Wiki hii tumeona kwenye Video vijana wamefanya makosa makubwa ya kujirekodi na kumtusi Rais ,katika maisha yangu ambayo nina zaidi ya miaka sabini sijawahi kuona maneno hayo hatakama tumepata uhuru kiasi gani,nilipoyaona niliwasiliana na viongozi wa jamii ya vijana ,nilichokifanya ni kuwaomba polisi  wasiwakamate ili tukayamalize l kimila walinikubalia"


"Kuanzia leo kijana arakayeonekana amesuka rasta apewe adhabu kali ninachotaka wasuke rasta za kimasai zinazokubalika atakayeonekana aletwe hapa na apigwe fimbo sabini,wale wanaovaa mlegezo na msichana anayepasua nguo hadi sehemu za siri ashughulikiwe na akina mama,tabia hii ikiachwa  itazalisha vijana wanaotukana wakuu wa nchi"


Katika hatua nyingine Meijo ametoa onyo kali kwa watu ambao wanataka kuvamia eneo lao la mila ambao walilimega na  kuzungushia uzio (fence) bila kufuata utaratibu. 


"Eneo hili la Eleray ni eneo la kupata mafunzo kwa vijana wawe na adabu tulivunja uzio uliozungushiwa hapa baada ya watu kutaka kuuza eneo hilo ambalo ni mali yetu, hatukubali wamasai hatupimwi wala hatutingishwi , kama kuna mtu anautajiri ajaribu kupimana na wamasai,ukija na pesa zako huingii hapa atakayeingia hapa ni rais Samia tu hapajengwi kitu hapa"


Kiongozi huyo aliwasihi wamasai kushiriki kikamilifu uchaguzi wa Oktoba mwaka huu ili kwenda kuchagua viongozi bora wanaowataka kwa ajili ya maendeleo yao.








ends...









Post a Comment

0 Comments