MGOMBEA UDIWANI OLASITI ATOA TAMBO ZA USHINDI BAADA YA KUTEULIWA RASMI
Na Joseph Ngilisho- ARUSHA
HALI ya shamrashamra na nderemo ilitawala mapema leo katika Kata ya Olasiti, jijini Arusha, baada ya mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alex Martin, kuchukua fomu ya uteuzi wake rasmi, akifuatana na umati mkubwa wa wanachama na wafuasi wa chama hicho.
Martin ambaye alikuwa akitetea kiti chake cha udiwani, awali alishindwa kwenye kura za maoni, lakini baadaye jina lake lilipendekezwa na Kamati Kuu ya CCM kutokana na vigezo mbalimbali ikiwemo uadilifu, utendaji wake na mchango mkubwa katika maendeleo ya kata hiyo.
Aidha Martin alisema Olasiti bado inamhitaji na alishukuru mchakato uliofanyika kuanzia Ngazi ya wilaya , Mkoa hadi Taifa ambao ndio wamerejesha jina lake baada ya mchakato mkali na hivyo alisisitiza kuwa yeye ni diwani wa kitaifa .Amewataka wananchi wa Olasiti Kutembea vifua mbele kwa kuwa mtetezi wao bado U hai.
>
“Najua tumepitia changamoto kwenye mchakato wa kura za maoni, lakini chama kimeona bado nina jukumu la kuwatumikia watu wa Olasiti .Nawaahidi sitawaangusha, bali nitaongeza kasi ya maendeleo, huduma bora na mshikamano wa wananchi,” alisema Martin huku akishangiliwa na umati wa wafuasi wake.
Ends ..
0 Comments