MPINA AGONGA MWAMBA TENA, MSAFARA WAKE WAZUIWA NA KUNDI LA POLISI MAGETI YAFUNGWA AKIREJESHA FOMU INEC!

 MSAFARA WA MPINA WAZUIWA KUINGIA MAKAO MAKUU YA INEC

Arushadigtal -DODOMA

 

MSAFARA wa Mgombea ubunge kupitia chama cha ACT wazalendo, Luhaga Mpina, leo ulijikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya Ofisi za Tume  huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) jijini Dodoma, wakati alipowasili kwa ajili ya taratibu za kurejesha fomu za kugombea nafasi ya urais.


  

Mashuhuda waliokuwepo eneo hilo walisema msafara wa Mpina ulivuta hisia za wananchi wengi, huku wafuasi wake wakiwa wamejitokeza kwa wingi wakipiga nderemo na kuimba nyimbo za kumtia moyo. Hata hivyo, ghafla walikumbana na askari waliokuwa wakisimamia ulinzi na kuambiwa wasitishe kuingia ndani ya eneo la INEC.


Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kizuizi hicho, mmoja wa viongozi wa msafara huo alisema:

> “Tulikuja kwa amani, nia yetu ni kumpeleka mgombea wetu kurejesha fomu. Lakini tulishangaa kuona tunawekewa vikwazo ambavyo havikustahili.”


Baadhi ya wananchi waliokuwa eneo la tukio nao hawakusita kueleza hisia zao.
Mzee mmoja aliyejitambulisha kama Mzee Sospeter, alisema:

> “Hii si mara ya kwanza kuona misafara ya wagombea urais, lakini kitendo cha kuzuiwa kurejesha fomu kwa mgombea wetu kimeleta tafsiri tofauti. Hata hivyo tunatarajia kila kitu kiende kwa amani.”


Mwananchi mwingine, Bi. Rehema, aliongeza:

> “Kwa kweli tulihamasika kuja kumsindikiza, lakini hali hii imeleta maswali. Tunachoomba ni amani na haki katika mchakato huu wa uchaguzi".

Tukio hilo limezua mjadala mpana katika mitaa ya Dodoma, wengi wakijiuliza iwapo hatua hiyo ilikuwa ya kiusalama pekee au ina tafsiri za kisiasa. NEC bado haijatoa tamko rasmi kuhusu kadhia hiyo.

Msafara wa mgombea wa urais wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina amezuiwa kuingia katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Dodoma.


Askari waliokuwepo kwenye ofisi hizo wamelifunga geti la ofisi hizo ili Mpina na wenzake wasiweze kuingia ndani.


Jana jumanne agosti 26,2025, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ramadhan Kailima alimwandikia barua Katibu Mkuu wa chama hicho ikieleza kwamba  Mpina  hatapaswa kufika katika ofisi za Tume kwa ajili ya uteuzi uliopangwa kufanyika leo Jumatano, Agosti 27, 2025.


Ends..

Post a Comment

0 Comments