MKE ADAIWA KUFIA KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI (GUEST🏠) VURUGU ZAIBUKA NYUMBANI
By Arushadigital
Hali ya mvutano imetokea katika mtaa wa Olmokeya, kata ya Sinoni jijini Arusha, baada ya ndugu wa marehemu Paulina Lohii kudai mwili wa mtoto wao ili wakazike Wilayani Mbulu mkoani Manyara, kufuatia kifo chake kilichotokea Jumatatu kwenye nyumba ya kulala wageni (Guest) katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya kutatanisha.
Ndugu wa upande wa marehemu wanataka kumzika kwao Mbulu kwa sababu mwanaume aliyekuwa akiishi naye tangu mwaka 2009 hakuwa ametoa mahari, licha ya uhusiano wao kujulikana pande zote mbili.
Kwa upande wake, mume wa marehemu, Joseph, amesema kuwa mke wake alikuwa na tabia ya kuondoka mara kwa mara, na siku ya tukio aliwaacha watoto wao nyumbani kabla ya kutoweka.
Ameeleza kuwa alipokwenda polisi kutoa taarifa, alielezwa kuna mwanamke aliyefariki kwenye nyumba ya wageni, na baada ya kufika mochwari alithibitisha kuwa ni mkewe Paulina.
0 Comments