By arushadigital-Dar
Rais Mstaafu wa Tanzania na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema utaratibu uliotumika kumuidhinisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM haujakosewa na kwamba ndio utaratibu uliotumika kuwapitisha na kuwaidhinisha Wagombea wote wa Urais wa Chama hicho tangu kuanza kwa mfumo wa Vyama vingi nchini.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo leo Alhamisi August 28, 2025 wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi Mkuu wa Tanzania.
“Najua kulikuwepo na vijineno eti utaratibu umekiukwa na Mimi nililaumiwa kwa jinsi nilivyosema pale kwenye mkutano mkuu lakini nasema waliokuwa wanayasema hayo ama hawafahamu utaratibu wa Chama chetu na kama wanafahamu labda wamesahau au wanajifanya hamnazo”
“Tangu tulipoanza mfumo wa Vyama vingi ndani ya CCM tumejiwekea utaratibu kuwa Rais wetu aliyopo madarakani anapomaliza kipindi cha kwanza na akataka kipindi cha pili huwa anapewa nafasi pekee yake, ndivyo ilivyokuwa kwa Rais Mkapa, ndivyo ilivyokuwa kwangu na ndivyo ilivyokuwa kwa Rais Magufuli, kwanini leo kuwe na kelele za kutaka iwe tofauti kwa Rais Samia, sababu yake nini!?”
“Mbona haya hatujayasikia kwa Mkapa, kwa Kikwete wala kwa Magufuli?, na kinachonishangaza Mimi wale ambao wanayasema sana haya wana kimbelembele wao wenyewe walikuwepo wakati wa Mkapa, wakati wangu lakini leo wanataka kuwatia Wana CCM na Watanzania jakamoyo kwa jambo ambalo halipo, Chama kimeshajiwekea utaratibu wake na utaratibu mzuri, utaratibu huo uendelee na kuheshimiwa”
End....1
0 Comments