RC KIHONGOZI ATOA SIKU TATU KWA WAENDESHA PIKIPIKI WALIOFUNGA TAA KALI NA MILIPUKO YABKUSHTUA WAONDOE BAADA YA HAPO KUKIONA!

 Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 

Kupitia

MKUU wa Mkoa wa Arusha ,Kenani Kihongosi  ametoa siku tatu kwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kuondoa fataki walizofunga kwenye pikipiki zao, zinazosababisha kelele za kushtua, pamoja taa zenye mwanga mkali  ambazo zimekuwa ni kero kwa wananchi pamoja na watumiaji wa usafiri huo.

Kihongosi ametoa rai hiyo leo Julai 22,2025 wakati akiongea na waendesha pikipiki na Bajaji katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeidbkarume  kuhusu kero hiyo inavolalamikiwa na wakazi na watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri kwenye maeneo yote ya mkoa huo.


"Nimeletewa kero hii na wazee na viongozi wetu wa dini, unapopiga fataki hiyo kumbuka kelele hizo zinaleta kero kubwa kwa watu wanaosikia, kuna wagonjwa, kuna wazee na wengine wenye shida nyingine, fanyeni utaratibu wa kuondoa kifaa hicho kinachotoa kelele yenye kero, hivyo natoa siku 3 kama, mlivyokubaliana hapa".Alisema


Pia aliwataka madereva hao, kuheshimu na kuithamini kazi yao, kwa kuwa ni kazi kama kazi nyingine inayowaingizia kipato na kuendesha maisha yao na familia zao, hivyo amewasihi kuhakikisha wanaendesha vyombo hivyo vya moto kwa kuzingatia sheria na taratibu pamoja na kutumia fedha hizo kwa ajili ya maendeleo.


"Tumieni kazi yenu kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, tumieni fedha vizuri kwa kuwa na malengo ya kimaendeleo, nyinyi ni vijana  twendeni, twendeni tukafanye maendeleo.hakikisheni 


Aidha, amewataka kuwa chanzo cha usalama wa mkoa wa Arusha kwa kuwa wao wapakia watu wa aina tofauti, na kuwataka kutoa taarifa za uhalifu kwa vyombo husika, kwa kuweka uzalendo mbele badala ya kudanganywa na kujihusisha na uhalifu na sio kuwa sehzmu ya uhalifu


Kazi hii mnayoifanya inatakiwa kuwapa kipato nyie na heshima ya Taifa hili, lindaneni ninyi kwa ninyi, wapo wageni wa ndani na nje ya nchi wanaotumia usafiri huu wa bodaboda, fanyeni kazi hii kwa ndihamu na weledi mkubwa.


"Wanaofanya biashara haramu ya tatu mzuka waache mara moja, heshimuni kazi yenu ili wengine waiheshimu, Serikali inaithamini kazi yenu ya usafirishaji, wanaokwenda kinyume hawatakuwa salama"




Ends...

Post a Comment

0 Comments