RC KIHONGOSI AONGOZA MAMIA MAZOEZI ARUSHA AKIMBIA KILOMETA 10,TAZAMA ALIVYOBURUDISHA KWA KUCHANA MISTARI NYIMBO ZA WASANII

Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 

MKUU wa Mkoa wa Arusha,Kenan Kihongosi ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Arusha kushiriki uzinduzi wa klabu ya mazoezi ya pamoja  (Jogging sport club) iliyofanyika katika viwanja vya ofisi hiyo.


 
Akiwa katika mazoezi hayo mapema leo julai 19,2925, yaliyotanguliwa na mbio za kilomera 10 na kushirikisha taasisi mbalimbali za umma jiji hapa,mkuu huyo wa Mkoa aliwaomba wananchi kujitokeza katika mazoezi yatakayofanyika kila jumamosi kwa lengo la kuboresha afya ili kuondokana na maradhi nyemelezi.

"Jambo hili litakuwa ni kila jumamosi tutafanya mazoezi kuondoa magonjwa yasiyoambukiza"

Pia alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa wakazi wa Arusha kuzingatia upendo ,umoja na mshikamano iwe nguzo ya Mkoa huo.

"Tukatae Majungu ,umbeya na unafiki,pia tukatae watu wanaogawanisha watu , tushirikiane,tuishi kwa upendo,maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana huna sababu ya kumchukia au kumuumiza yeyote kwa sababu kesho yako huijui"

"Kila mmoja hapa anafamilia yake,anashida zake na kila mmoja anawatu wanaomtegemea ndio maana siku zote tunasema usipande miba kwenye njia ya mtu kwa sababu siku moja utapita ukiwa pekupeku
 ikakuchoma"

















Ends..






Post a Comment

0 Comments