Na Joseph Ngilisho- ARUSHA
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi amemwagiza Mkurugenzi wa jiji la Arusha kuweka mazingira mazuri kwa watu wanaofanyabiashara kwenye mabaraza ya maduka ili kuacha kuwabughudhi wafanyabishara wanalipa kodi ya serikali.
Kihongosi ametoa agizo hilo leo Julai 22,2025 wakati akiongea na wamiliki wa saluni pamoja na wafanyakazi wao na kubaini changamoto zao na kutoa agizo hilo ikiwa ni njia ya mojawapo ya kutafuta suluhu na amani ya kudumu katika mkoa wa Arusha.
Alisema kumekuwepo na malalamiko kwa wafanyabishara wa saluni wakidai kuvamiwa na wasusi wanaokaa vibarazani kiasi cha kuwabughudhi kwenye biashara zao halali na hivyo alimwagiza mkurugenzi wa jiji na afisa biashara wake kutafuta suluhu ya jambo hilo ilib wafanyabiashara wasibughudhiwe .
"Maeneo ya biashara za watu hata mimi huwa sifurahiwi kuona mtu mwingine anafanya biashara juu ya mwingine wakati huyo analipa kodi ya serikali ,ninamwagiza mkurugenzi kuona namna ya kutatua hili jambo kwa kuweka utaratibu mzuri ili kila mtu apate riziki yake"
Aidha alisisitiza kwa wafanyabishara hao kuilinda amani ya nchi kama tunu pekee inayostahiki kulindwa kwa watu mbalimbali na kusisitiza vijana wasikubali kurubuniwa na kuipoteza amani iliyopo kwani baadhi ya watu wakiona wameharibu amani iliyopo wabakimbilia nchi za nje na kuacha wenzao wakitaabika
"Tulinde amani ya nchi yetu na tusikubali kurubuniwa na hao wanaoleta uchochezi lakini wanaona Rais Samia Hassan Suluhu ni mwanamke wanaamua kusema hajafanya kitu hivi nyie kazi zilizofanywa na Rais hamzioni ?miradi ya kimkakati imetelelezwa ikiwemo reli ya SGR , bwawa la Nyerere na mingineyo sasa wasiopenda maendeleo kazi zao kupinga ila wenye akili kazi z unaonekana"
Alisema watu wa saluni ni kada nzuri yenye wateja wengi hivyo wanapoona kunahabari tofauti za wateja wao watoe taraifa serikali ili hatua ziweze kuchukuliwa na kusisitiza kulinda amani kwa kutoa viashiria ambavyo havijakaa sawa kwani amani ya nchi ni tunu pekee.
Alisisitiza waajiri wa saluni kutoa mikataba ya ajira huku alisema Jiji la Arusha linash, bilioni 5.5 kwaajili ya utoaji mikopo ya asilimia kumi inayotolewa serikali kwa vijana, wanawake na makundi maalum kwaajili ya kupata mikopo hiyo ili wajikwamue kiuchumi ambapo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John Kayombo alisisitiza elimi hiyo kuendelea kutolewa ili watu mbalimbali waweze kupata mikopo.
Katika mkutano huo, masuala mbalimbali yaliibuliwa na kujadiliwa kwa uwazi. Miongoni mwa mambo yaliyopewa uzito ni pamoja na
Changamoto za usajili wa biashara na upatikanaji wa vibali.
Hitaji la mafunzo ya usafi wa mazingira ya kazi na usalama wa vifaa.
Kupandisha viwango vya huduma ili kuendana na ushindani wa kibiashara.
Wamiliki wa saloon na (barbershop) walipata nafasi ya kuelezea hali halisi ya biashara zao, huku wengi wakieleza changamoto wanazokumbana nazo, hasa kwenye masuala ya ushuru, uelewa wa sheria, na mazingira ya kazi.
Mkutano huo ulihitimishwa kwa makubaliano ya kuandaliwa kwa mafunzo maalum kwa wajasiriamali hao, pamoja na kusimamiwa kwa karibu na serikali ili kuhakikisha huduma bora kwa wateja na kukuza ajira kwa vijana.
Kihongosi aliwaahidi wamiliki wa saloon na barbershop kuwa serikali ipo tayari kushirikiana nao, na akasisitiza kuwa hatapendelea kuona biashara yoyote inafungwa kwa sababu ya kukosa elimu au taarifa muhimu kuhusu uendeshaji wa shughuli zao.
Baadhi ya wamiliki wa saluni, walieleza kero mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wakiendesha biashara hiyo ikiwemo suala la leseni pamoja na wafanyabishara wa vipodozi wanaofanya biashara ya ususi kwenye vibaraza vya maduka yao na kuwanyima kipato saluni zenye usajili na zinalipa kodi.
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji Jiji la Arusha John Kayombo, ameweka wazi kuwa kwa sasa Jiji hilo linazo shilingi Bilioni 5.5 fedha za mapato ya ndani zilizotengwa kwa ajili ya mikopo isiyokuwa na riba kw a makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu na kuwasisitiza wakazi wa Jiji hilo wenye sifa kwenda kukopa pesa hizo.
Ends...
0 Comments