MAGIGE AANGUKIA PUA UBUNGE VITI MAALUMU ARUSHA WAJUMBE WAMDUWAZA ,ATOKA NDUKI UKUMBINI BILA KUSAINI MATOKEO
By Arushadigital
ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha Catherine Magige ameshindwa kutetea nafasi yake na kujikuta akitoweka ukumbi bila kuaga wala kusaini matokeo wala kutoa neno la shukrani kwa wajumbe waliompatia ridhaa hiyo kwa kipindi tofauti kwa miaka 20.
Katika uchaguzi huo uliokamilika maiira ya saa tano usiku leo Julai 30,2025, Magige alishika nafasi ya tatu kati ya wagombea nane na kuambulia kura 213.
Anadaiwa kutoweka ukumbini wakati kura zake zikimalizikia kuhesabiwa katika mchakato wa kusaka wawakilishi wa wawili wa Ubunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha .
Katika hali ya kushangaza baadhi ya wajumbe kwa uchache walionekana kumzonga kwa kumfuata nyuma huku wakiimba nyimbo za kumkejeri .ambapo alionekana kupandwa na jazba na kuanza kuwatolea maneno makali yasiyoandikika hewani huku akisikika akisema "nimewanunulia vitenge vyangu hamna shukrani
Kando na hilo Magige alionekana kupiga simu ngazi za juu kuomba msaada akilalamikia mwenendo wa uchaguzi huo akidai haukuwa huru na haki jambo lililomchefua msimamizi wa uchaguzi huo Kenani Kihongosi mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Katibu wa ccm Mkoa Musa Dadi Matoroka.
Katika kinyang'anyiro hicho MARIRTA KIVUGE alipata kura 1004 na kufuatiwa na CHIKU ISSA aliyepata kura 775.Wengine waliofuatia kwa mbali ni ASANTE RABI LOWATE 196, ZAYTUN SWAI 141,NAVSI AMO 50 na LILIAN BACHI 9.
Ends..
0 Comments