NA Joseph Ngilisho- ARUSHA
BAADA ya ukimya wa takribani Miaka miwili Leo Julai 1,2025 aliyekuwa mkuu wa wilaya ya HAI ,Lengai Ole Sabaya, ameingia Rasmi katika mbio za kulitaka Jimbo La Arumeru magharibi na kuongeza joto la kinyang'anyiro cha uchaguzi baada ya kunyakua Fomu ya Uteuzi.
Ole sabaya akiwa na Mke wake Jesca Thomas amefika Katika Ofisi za Ccm wilaya ya Arumeru na kukabidhiwa Fomu na Katibu wa ccm Camilla Kigosi kwa ajili ya Kuomba Ridhaa ya kuteuliwa na chama chake kupeperusha bendera ya jimbo linaloshikiliwa na mbunge anayemaliza muda wake Noar Lembris.
Sabaya anatazamwa kama Mwanasiasa Machachari asiyechoka mwenye haiba ya upole ba mchapakazi, kijana mwenye msimamo mkali wenye faida,aliyepitia milima na mabonde ya Siasa.
Sabaya ameleta Joto na mtikisiko mpya ndani ya jimbo hilo ,huku akiwaweka katika wakati mgumu wagombea wenzake ndani ambao wameonyesha awali nia ya kulitaka jimbo hilo akiwemo Mbunge wa sasa Noah Saputu,Na aliyekua mwenyekiti wa wilaya wa Ccm Noel Severe na wengine.
Majira ya saa 10 Mwamba huyo akiwa ameambatana na mke wake alitonga katika ofisi ya ccm iliyopo Sekei na kupatiwa Fomu ya kuwania uteuzi wa ubunge.
Alipotakiwa kuongea na vyombo vya habari vilivyopiga kambi ofisi ccm Arumeru baada ya kupata tetesi kwamba angefika kuchukua fomu, Sabaya ameonekana kutokuwa tayari kuongea akisema “Namuachia Mungu aifanye kazi yake
”
Hata hivyo Sabaya hakutaka kuzungumza chochote zaidi ya kusema anamwachia mungu atende kazi yake.
Sabaya aliwahi kuwa diwani wa kata ya sambasha,Ndani ya jimbo hilo huku akishinda katika kipindi cha mtikisiko mkubwa wa ushindani na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ,anatajwa kama mwanasiasa mwenye nguvu na ushawishi mkubwa kwa wananchi.
Pia Uwezo wake wa kujenga hoja,sifa ya Udhubutu na uzoefu katika siasa za uchaguzi,pamoja na siasa za hamasa, zinatajwa kama sababu zinazompendelea Ole sabaya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana mkoa wa Arusha na Mkuu wa wilaya ya Hai.
Katika Jimbo La Arumeru magharibi lenye kata 27,na wajumbe takribani elfu 13 wa ccm wanaopiga kura,ni wazi kwamba kitu pekee kinachompendelea mgombea ni sifa ya uwezo wa kujenga hoja sifa ambayo watu wa makundi mbali mbali wanakiri kwamba Kama Ccm itamteua,basi sabaya ana sifa hiyo.
Hii ni Mara ya Kwanza kwa Sabaya kuonekana Hadharani akifanya shughuli za kisiasa tangu kutoka Gerezani kwa kushinda kesi zilizokuwa zinamkabili.
Ujio wa sabaya utachochea Joto la siasa za kanda ya kaskazini kwa wanasiasa vijana na machachari wanaoomba kuaminiwa na Chama cha mapinduzi kuteuliwa wakiwemo aliyekua mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda anayeomba kuteuliwa Katika jimbo la Arusha na Joshua Nasari aliyeomba kuteuliwa katika jimbo la Arumeru mashariki.
Hadi kufikia Leo Julai,1 2025,Takriban wagombea zaidi ya 20 walikuwa amemimika kuchukua fomu wakiwemo wanawake watano.
Ends.
0 Comments