Na Joseph Ngilisho-ARUSHA
WAKULIMA wa mbogamboga na matunda kutoka Mikoa ya Arusha Kilimanjaro na Manyara ,wameanza kunufaika na soko la uhakika la mazao yao mara baada ya kufunguliwa kwa kiwanda cha kuchakata na kufungasha mazao ya Mbogambona na matunda cha Nurusafe kilichopo Kisongo wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Hayo yamebainishwa leo julai 8,2025 na meneja wa kiwanda hicho,Okuli Meena wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kiwanda hicho cha News Nurusafe Packhouse, chenye ushirikiano na KOICA & CAST kutoka nchini Korea Kuzinduliwa na mbio za Mwenge Mwaka 2025.
Meena alifafanua kwamba ,tangu kuanzishwa kwa mradi huo Januari mwaka huu,2025 wakulima kutoka Mikoa ya Njombe , Kilimanjaro,Manyara wamekuwa wakiuza mazao yao na kulipwa fedha tasilimu bila usumbufu wowote.
"Kiwanda chetu kipo kisongo katika halmashauri ya Arusha,Hapa tunahusika na uchakataji na ufungashaji wa mazao ya Mbogambona na mazao mengine na tunahitaji wakulima wa mazao hayo walime kwa wingi kwa sababu soko la uhakika lipo"
Alisema mazao yanayochakatwa katika Kiwanda hicho ni pamoja Maharage Machanga(Green Beans),Karela au Tango Pori(Better Gurd)Njegere Changa,Parachichi(Avocados) na Bilinganya.
"Wakulima wengi walikuwa wanalima mazao ya Mbogambona na hawajui wanaenda kuuza wapi, lakini baada ya kuanzishwa kwa mradi huu wakulima wengi wamehamasika kulima kilimo cha Mbogambona"
Alisema wakulima wa mazao hayo wamekuwa wakiongozwa na wasafirishaji kulima mazao yanayohitajika na hivyo kuwa na uhakika na soko la biashara kwa mazao wanayolima.
"Katika jengo hili mkulima hapotezi mazao yake huwa tunahifadhi mpaka soko linapokuwa zuri iwapo inatokea biashara ya mazao kitokuwa nzuri kwa wakati huo"
Akiongelea suala la ajira alisema kuwa kiwanda hicho kimechangia ajira kwa kiasi kikubwa mpaka sasa watu zaidi ya 160 wamepata kazi na miongoni mwao 80 wamepata ajira za moja kwa moja.
Alisema katika mradi huo Wafanyakazi , wanaofanya kazi kwa kupokezana kwa awamu mbili kila siku
Ends ..
0 Comments