Na Joseph Ngilisho- ARUMERU
CHAMA Cha Mapinduzi katika jimbo la Arumeru Magharibi kimeanza mchakato wa mchujo kwa watia nia 22 walioomba nafasi ya ubunge katika jimbo hilo mara baada ya kuwaita na kuwahoji kwa kina nia yao ya kulitaka jimbo hilo ili kumpata kiongozi wa dhati mwenye uwezo wa kutumikia wananchi.
Aidha kimewahalikishia wananchi wa jimbo hilo kuwaletea Mgombea Bora mwenye uwezo mkubwa kuwaletea maendeleo na kuondoa changamoto zilizopo katika jimbo hilo.
Akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu kwa watia nia 22 wa jimbo hilo,Katibu wa siasa na uenezi na mafunzo wilayani humo, Nicolaus Sawa alisema kuwa jimbo hilo limekuwa na watia nia bora na wanauhakika kupata mgombea sahihi mwenye uchu wa maendeleo.
Sawa alisema kuwa uongozi wa ccm leo ulikutana na watia nia wote;22 kwa lengo la kufahamiana pamoja na kuanza kwa mchakato wa mchujo ili kupata wawakilishi watatu ambao watapigiwa kura na wajumbe kwenye kata mbalimbali za jimbo hilo.
Aidha aliwaonya watia nia hao wakati wa kampeni za chama kutotumia Lugha zinazotweza utu wa mwingine badala yake waombe kura kistaarabu kwa kunadi sera zao kwa wajumbe.
Pia alisema jimbo hilo limekuwa ma mwitikio wa wagombea wa viti Maalumu katika Tarafa tatu za jimbo hilo ,Tarafa ya Enaboiishi wanawake 19,Tarafa ya Mukulati 13 nanTarafa ya Moshono wanawake 7.
"Leo tumekutana na watia nia wote 22 wa ubunge wakiwemo wanawake watatu kwa lengo la kuwafahamu ikiwa ni pamoja na kufahamu nidhamu zao na uhalali wao ndani ya chama"
"Sisi kamati ya siasa wilaya ya Arumeru tutawaletea wagombea bora sana mtawasikia wenyewe wakati wakijinadi kuomba kura kwa wajumbe"
Sawa aliwahikikishia watia nia kwamba hakutakuwa na upendeleo katika zoezi la mchujo na watazingatia zaidi sifa za ziada za mtia nia .
Ends..
0 Comments