MAREKANI YAICHAPA IRAN YAANGAMIZA VITUO VYAKE VITATU VYA NYUKLIA,YASUBIRI AYATOLLA RAIS WA IRAN AJIBU ISHUSHE KIKOSI CHA MAANGAMIZI

 By Arushadigtal

Ndege za kivita za Marekani zilisafiri kwa zaidi ya saa 37 kutoka Marekani hadi Iran kwa ajili ya kutekeleza shambulizi dhidi ya vituo vitatu vya kinyuklia nchini humo.


Akisisitiza kwamba operesheni hiyo haikuway a kuondoa mamlaka inayoonogozwa na Ayatolla Khamenei, Waziri wa ulinzi wa Marekani amesisitiza kwamba juhudi hii ya kivita ilikuwa ya kuondoa tishio la kinyuklia ambalo Iran ilikuwa nayo.


“Rais Trump alisisitiza kwamba aliipa Iran siku 60 kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kuafikiana katika makubaliano kudhibiti uwezo wao wa kuw ana silaha ya kinyuklia. Iran kamwe haiwezi kukubaliwa kumiliki silaha hizo,” Pete Hegseth aliwaambia wanahabari katika makao makuu ya jeshi la Marekani ya Pentagon katika kikao cha wanahabari.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Majeshi ya Marekani Jenerali Dan Caine, ndege saba za aina ya B2 spirit bomber zilitumwa Iran na kutekeleza shambulizi lililotekelezwa kwa usiri mkubwa ambao lilipata jeshi la Iran likiwa halina taarifa za awali kuliwezesha kuzuia ndege hizo kupaa kwenye anga yao.


Jenerali Caine anasema kwamba vituo vyote vitatu vya kinyuklia vililengwa mwendo wa saa nane usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki na vile vile Iran yenyewe.


Maeneo ya nyuklia ya Iran 'yameharibiwa vibaya' baada ya mashambulizi, amesema.


Makombora aina ya TOMAHAWK yalikuwa ya mwisho kurushwa katiak kituo cha Isfahan kuhakikisha kwamab Marekani imedhibiti hali ya kuwashtuwa WaiIrani katika operesheni iliyojumuisha majeshi yake ya angani na ya majini.


Kabla ya mabomu kurushwa kutoka kwenye ndege za kivita, makombora kadhaa yalirushwa na jeshi na majini la Marekani kutoka kwa boti maalum lenye uwezi wa kuzama ndani ya Bahari lililokuwa baharini.


Katika operesheni hiyo jeshi la Marekani lilirusha mabomu 14 kwenye vituo viwili vikuu vya Fordo na Nantanz , huku serikali ya Marekani ikisema kwamba tathmini ya awali ni kwamba maeneo yaliyolengwa yaliharibiwa vibaya japo ni mapema sana kujuwa ikiwa uwezo wa kinyuklia wa Iran umemalizwa kabisa.


Marekani imesisitiza kwamba ikiwa Iran italipiza kisasi basi jeshi al Marekani litajibu kwa ukali huku kambi zake za kijeshi katika mataifa ya Iraq, Bahrain, Qatar na Syria zikijiandaa kwa choctote kile.

Post a Comment

0 Comments