Na Joseph Ngilisho- ARUMERU
MHADHIRI wa TEHAMA Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,Mathew Mndeme amejitosa kuwania Ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki akiwa na lengo la kuleta mabadiliki chanya ya maendeleo kwa jamii iwapo atapata ridhaa ya kuteuliwa.
"Nimechukua fomu kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki nikiwa na shauku ya kuleta maendeleo chanya katika jamii ukizingatia kwamba jimbo hili lina fursa zingi za kiuchumi lakini zimekuwa haziwanufaishi wananchi wake"
"Nimefanya tathmini ya kina juu ya uwezo wangu, nimejiridhisha kuwa nina kila sababu na sifa zinazohitajika kuwatumikia wananchi wa Arumeru Mashariki katika ngazi ya ubunge.” Alisema Mndeme!
Dkt Mndeme mwenye shahada ya Phd na mkazi wa Njani ,Nkoaranga Arumeru Mashariki,amejitosa kuwania uteuzi ndani ya CCM akiwa na maksudi matatu ya kuleta mabadiliko ya uongozi wenye tija ili kusaidia jimbo hilo.
"Nimefanyakazi kwenye sekta ya TEHAMA kwa zaidi ya miaka 20 nikiwa nimebobea na kuwa na shahada ya nne ninaimani nikipata idhini ya kugombea ubunge nitawasaidia sana wananchi pamoja na taifa langu kuchochea maendeleo"
Ends .
0 Comments