DABI YA SIASA YAHAMIA NGARENARO KIJANA AMKABA KOO DIWANI ALIYEMALIZA MUDA WAKE,ASEMA HATISWI NA VITISHO VYAKE ,AVUNJA MWIKO WA KUWATISHA WASIGOMBEE KATIKA KATA HIYO ETI KATA INA MWENYEWE!

Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 

KADA Kijana wa CCM Kata ya Ngarenaro jijini Arusha, THABITI ABRAHAMAN NASAOR amejitosa kuchukua Fomu ,kuwania Nafasi ya Udiwani katika kata hiyo kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi walioteseka kwa muda mrefu bila kuwa na mwakilishi sahihi mwenye kujua shida za watu.


Thabiti ambaye aliwahi kuwa katibu wa siasa na uenezi katika kata hiyo amemtaka Diwani aliyemaliza muda wake kupumzika na kuacha damu changa zishike hatamu kwani mchezo wa kisiasa hauhitaji hasira.

 , Alisema ameamua kutumia haki yake ya msingi kugombea nafasi hiyo kama mchakato ulivyotangazwa ili kuvunja mwiko uliozoeleka wa kutishwa kuwa kata hiyo  ina  mwenyewe haigombewi.


Akiongea mara baada ya kuchukua Fomu leo Juni 30,2025 ,alidai kwamba diwani aliyemaliza muda wake ISAYA DOITA amejimilikisha kata hiyo kiasi cha kuwatisha makada wengine wasijitokeze kugombea nafasi hiyo jambo ambalo yeye amelipinga kwa nguvu zote akidai ameamua  kuvunja mwiko huo.

"Kama mnavyofahamu nagombea kwenye kata ambayo wapo baadhi ya viongozi ndani ya chama ambao wamejimilikisha wakidai kata hiyo inamwenyewe ,mimi nimeamua kuchukua fomu ili kugombea nafasi hiyo kwa kujibu wa taratibu za chama chetu "

"Kwa hiyo ndugu zangu najua nitakutana na changamoto mbalimbali baada ya kutangaza kugombea nafasi hiyo ninachosema nimejipanga, nimejitathimini kuwa naweza kuitumikia jamii,najua baada ya kutoka hapa nitakumbana na vitisho wakihoji v nani amekutuma kuchukua fomu, mimi sitaogopa vitisho "

Alisema kuwa ametumika ndani ya chama hicho kwa miaka 13 amepata uzoefu wa kutosha ni wakati wa kwenda kuonyesha uwezo wake kwa kuwatumikia wananchi kama kijana mwenye damu changa inayochemka.

Ends.

Post a Comment

0 Comments