KISHINDO CHA SABAYA AKICHUKUA FOMU UBUNGE JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI, VIONGOZI WAMILA NA DINI WAMIMINIKA KUMWOMBA AGOMBEE!

 Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 


IKIWA idadi ya wanaopigania ubunge jimbo la Arumeru Magharibi wakifikia 20,hofu imetanga kwa baadhi ya watia nia kufuatia kuwepo fununu za aliyekuwa mkuu wa wilaya ya HAI LENGAI OLE SABAYA KUTINGA katika kinyang'anyiro hicho akilitaka jimbo hilo kwa udi na uvumba.

Sabaya baada ya kumaliza misukosuko na mahakama kumsafisha ,aliamua kukaa kimya alijiimarisha kisiasa ila kwa sasa ameona ni wakati mwafaka wa kutumika kisiasa, kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kama mbunge aliyepenya akitokea kwenye udiwani na baadaye kuwa DC wa HAI Mikoani Kilimanjaro.

Sabaya ambaye amekuwa tishio na mwiba mkali kisiasa na huenda  akawatingisha vigogo kadhaa waliokwisha chukua fomu kuwania uteuzi katika jimbo hilo.

Ukimya wa Sabaya Si haba unakishindo hasa baada ya wananchi katika jimbo  kuonesha wazi bila kuficho  wakimhitaji baada ya kufuatwa  na watu mbalimbali wakiwemo wazee wakubwa na watumishi wa mungu walimwomba agombee nafasi hiyo.

Kwa mujibu katibu wa ccm wilaya ya Arumeru ,Camilla Kigosi,makada wapatao 20 wamechukua fomu na baadhi kurejesha kwa lengo la kuwania kugombea ubunge katika jimbo hilo


Post a Comment

0 Comments