BAYO MWENYEKITI MPYA TAMONGSCO TAIFA, AMGARAGAZA VIBAYA MTETEZI WA NAFASI HIYO,APANGA MIKAKATI MIZITO KUIMARISHA ELIMU BORA KWA SHULE BINAFSI!

Na Joseph Ngilisho-DODOMA


SHIRIKISHO la Wamiliki wa Shule Binafsi Nchini(TAMONGSCO)limemchagua  Mkurugenzi wa shule za Tumaini ,Modest Bayo kuwa mwenyekiti Mpya wa Taifa wa Shirikisho hilo kwa muda wa Miaka Mitano.


Bayo aliibuka kidedea baada ya kumwangusha mtetezi wa kiti hicho, Alfred Luvanda katika Mkutano Mkuu wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini uliofanyika jijini Dodoma.


Akiongea mara baada ya Kuchaguliwa kwa kishindo mapema mwezi huu june 11 ,2025 ,alisema alivutiwa kuomba nafasi hiyo kwa lengo la kuiweka karibu taasisi hiyo na serikali ili kuboresha sekta ya elimu hapa nchini ukizingatia kwamba TAMONGSCO ni shirikisho huru lenye mlengo wa kuleta ushindani wa elimu bora hapa nchini.


"Mikakati niliyonayo ni kuijenga shirikisho hili kutoka ngazi ya Taifa kwenda kuliimarisha ngazi za Kanda  , Mkoa na wilaya na nimevutiwa kugombea nafasi hii kwa lengo la kuleta Taswira mpya ya chama chetu cha wamikili wa shule na vyuo hapa nchini "


Alisema wao kama wawekezaji na wadau katika sekta ya elimu hapa nchini, wanao mchango mkubwa wa kutoa elimu bora na lengo lao ni kuendelea kushirikiana na serikali katika kutoa mawazi yao ili kujenga misingi imara ya kuimarisha elimu hapa nchini kwa kufuata  miongozo ya serikali.


"Moja ya mikakati tunayokwenda kuanza nayo ni kufanya mipango madhubuti ya muda mrefu, muda wa kati na muda mfupi ya kujenga misingi imara itakayowezesha  kuboresha elimu hapa nchini ili iwe na tija kwa kuwaunganisha wadau wa sekta ya elimu na wamiliki wa shule hapa nchini "Alisema Bayo!


Bayo ambaye ni Mmiliki wa shule za Tumaini Senior  iliyopo wilaya ya Monduli na Tumaini Junior iliyopo wilayani Karatu katika Mkoa wa Arusha alisema  kabla ya wadhifa huo alikuwa mjumbe mwakilishi wa TAMONGSCO katika ngazi ya Kanda,Mkoa na Wilaya  tangu Mwaka 2008 hivyo kuwa na uzoefu wa kutosha ndani ya shirikisho hilo.

Safu Mpya ya viongozi wa TAMONGSCO Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti Mteule Modest Bayo wa tatu kutoka kulia waliokaa.



Ends..



Post a Comment

0 Comments