Na Joseph Ngilisho-ARUSHA
KAMPUNI ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation ni miongoni mwa kampuni zilizotunukiwa vyeti vya udhamini uliowezesha Mafunzo ya mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Arusha.
Aidha uwepo wa kampuni hiyo katika mafunzo hayo ya mawakili wa serikali ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya kampuni hiyo na serikali.
Meneja Mkazi wa kampuni hiyo nchini , dk Melkiory Ngido alibainisha hayo leo June 3,2025 baada ya kampuni yake kutambulishwa na kupatiwa cheti katika mafunzo ya mawakili wa serikali yanayofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Arusha.
Alisema Kampuni hiyo yenye ubia na serikali inasimamia migodi mitatu nchini ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi imekuwa ikifanya vizuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na kuwa kinara katika sekta ya ulipaji wa kodi kubwa nchini.
"Ofisi ya wakili mkuu wa serikali ipo nasi kwa sababu inasimamia rasilimali za nchini ikiwemo migodi kwa sababu Madini ni mali ya serikali"
Alisema kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya kampuni hiyo imetambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa kulipa Kodi kubwa nchini kwa muda wa miaka miwili mfululizo na hivyo kujijengea heshima kubwa kutokana na ushirikiano na serikali.
"Tumefanya mabadiliko makubwa sana katika uwekezaji wetu kwani hadi sasa kampuni imeajiri asilimia 96 ya wafanyakazi ni wazawa na manunuzi ya ndani yameongezeka na kufikia asilimia 86"
"Sisi Kama Barrick tumefurahi kupata mwaliko huu ndio maana tumeshiriki kusapoti mafunzo haya ya mawakili wa serikali na hii ni baada ya serikali kutambua mchango wetu"
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa na waziri wa Katiba na Sheria dkt Damas Ndumbaro na yanatarajiwa kumalizika June 5,2025.
Ends..
0 Comments