KIMEUMANA CCM :MBUNGE WA CCM AMSHUKIA VIKALI MBUNGE MWENZAKE AMTUHUMU KUMKOSOA RAIS SAMIA

By arushadigtal


Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Abbas Tarimba amemshutumu vikali mbunge mwenzake wa chama tawala CCM kwa kukosoa juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan huku akiziomba mamlaka kumchukulia hatua.


"Kuna mtu mmoja humu ndani mwenzetu, mbunge, tena ana nafasi ya kuzungumza humu ndani, ana nafasi ya kuzungumza kwenye NEC, ana nafasi ya kukutana na wakubwa.. anaanza kutuchokonoa. Mimi nakiuliza chama changu CCM, huyu bwana ana kadi ya chama.. hivi tukae tuwe na mtu kama huyu ambaye anatusumbua..."


Hakuishia hapo Tarimba aliyeonyesha kukerwa na matamshi yaliyotolewa na Gwajima alipozugumza na waandishi wa habari juu ya masuala kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na utekaji, akaonya dhidi ya hatua ya mbunge mwenzake ya kutoa mifano mibaya dhidi ya familia ya rais Samia Suluhu Hassan. 


"...unakwenda kugusa familia yake, unagusaje familia yake, mtoto wake, unajua jinsi ya kupata mtoto wewe, unajua kulea? Unamtaja mtoto wake kipenzi kwamba akitobolewa macho? Mungu akulaani kabisa huko uliko. Na haya yasitimie kabisa." 


Unayazungumziaje matamshi kama haya na hasa yanapotolewa na viongozi wanapokosoana katika masuala yahusuyo taifa?

Post a Comment

0 Comments