KONGAMANO KUBWA LA KUMPONGERA RAIS SAMIA LAJA ARUSHA,VIONGOZI WA DINI KUMLILIA MUNGU

 Na Joseph Ngilisho Arusha 

Kongamano kubwa la kumpongeza Rais Samia Suluhu ,lililokuwa limepangwa kufanyika Agosti 5 mwaka huu ,limesogezwa mbele hadi hapo litakapotangazwa tena.

Kongamano hilo linaloandaliwa na taasisi ya dini ya Kiislamu ya Twarika mkoani Arusha kwa kushirikiana na viongozi wengine wa dini,linalenga kumpongeza na kumtia moyo rais Samia kutokana na kazi kubwa ya kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini.

Msemaji wa taasisi hiyo Sheikh Haruna Husein alisema sababu za kuahirishwa kwa kongamano  hilo ni kuboresha zaidi maandaliazi na limepangwa  kufanyika katjka hotel ya Golden Rose jijini Arusha.
"Tumesogeza  mbele Kongamano letu ili kuboresha zaidi maandalizi  ,sisi kama viongozi wa dini tunawajibu wa kumwombea na kumtia moya kiongozi wetu rais Samia na serikali yake  ili aweze kuongoza vizuri na kuwa na upendo wa taifa letu"

"Tunataka tumlilie Mungu katika jambo hili ili amjalie heri rais Samia kuliongoza vema taifa lake  na tunauhakika rais wetu ni msikivu ,mwenye Weledi na anaupendo na watu wake' 

Post a Comment

0 Comments