By Arushadigital-Dar
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, ameiambia mahakama kwamba hayuko tayari kuendelea na kesi yake ya uhaini inayomkabili hadi pale wanachama na wafuasi wake watakapokuwa wanaruhusiwa kuingia mahakamani.
Akizungumza mbele ya majaji watatu, Lissu amesema kesi yake inapaswa kusikilizwa hadharani, lakini maafisa wa polisi wamekuwa wakiwazuia wanachama wake kuingia mahakamani.
Ameomba mahakama itoe mwongozo wa haraka, kwa kuwa ni majaji pekee wanao mamlaka ya kutoa mwongozo wowote mahakamani kwa mujibu wa sheria. Baada ya hoja hiyo kuwasilishwa, Jaji Kiongozi Dastan Ndunguru ameahirisha kesi hiyo kwa muda na kusema watarejea kutoa maamuzi.
Jana kulitokea makabiliano kati ya baadhi ya polisi na wanachama wa Chadema nje ya mahakama.
Polisi walidai vurugu hizo zilisababishwa na wanachama waliokataa kufuata maelekezo yao.
Kesi ya Lissu inaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu, Masijala ya Dar es Salaam, huku kampeni za uchaguzi zikiendelea.
Chama chake kimesema hakitashiriki uchaguzi hadi mabadiliko ya sheria za uchaguzi yatakapofanyika.
0 Comments