Ad
Breaking🔥

LUKUMAY AHOJI UJENZI WA JENGO LA DHARURA OLTRUMENT, AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA SH, MILIONI 500

LUKUMAY AHOJI UJENZI WA JENGO LA DHARURA HOSPITAL YA WILAYA OLTRUMENT

....Apongeza Rais Samia kwa Sh milioni 500 za jengo la uzazi

Na Joseph Ngilisho | DODOMA

MBUNGE wa Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes  Lukumay, ameitaka Serikali kueleza itakapojenga jengo maalumu la huduma za dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya ya Oldonyo, akisema miundombinu hiyo ni muhimu katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Dkt. Lukumay aliuliza swali hilo Leo OKTOBA 29,2026 wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika Bunge linaloendelea jijini Dodoma, huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la huduma za uzazi (Maternity Complex) katika hospitali hiyo iliyopo Jimbo la Arumeru Magharibi.

Alisema uwekezaji huo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha miundombinu ya afya na kuongeza uwezo wa hospitali kutoa huduma kwa wananchi.

Hata hivyo, mbunge huyo alitaka kufahamu lini Serikali itaanza ujenzi wa jengo rasmi la huduma za dharura katika hospitali hiyo ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri alisema huduma za dharura zinaendelea kutolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Oldonyo, lakini Serikali itashirikiana na mbunge huyo kuhakikisha ujenzi wa jengo maalumu la huduma hizo unakamilishwa.

Alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha hospitali zote za wilaya zinakuwa na miundombinu inayohitajika na kutoa zaidi ya huduma 12 muhimu kwa wananchi.

Naibu Waziri aliongeza kuwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa na mbunge huyo, itaendelea kuhakikisha miradi ya afya inakamilishwa ili wananchi wapate huduma bora.

Alisema Serikali pia inaelekeza nguvu katika kukamilisha miradi ya vituo vya afya na zahanati ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchini.

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم