WANAFUNZI WATATU WA KIDATO CHA TATU WAFARIKI AJALI YA BARABARANI ARUMERU
Na Joseph Ngilusho-ARUMERU
Kamanda Masejo amesema ajali hiyo imetokea Oktoba 30, 2026, majira ya saa 11 jioni, ikihusisha lori aina ya Mercedes-Benz lenye namba za usajili T.415 DSN, lililokuwa likivuta tela lenye namba T.636 DSG.
Amesema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Abdul Seleman, mkazi wa Arusha, lilipoteza uelekeo na kugonga gari aina ya Toyota Rumion, lenye namba za usajili T.481 EKZ, lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara, kabla ya kuwagonga wanafunzi hao watatu waliokuwa wakitembea kwa miguu na kusababisha vifo vyao.
Kwa mujibu wa Kamanda Masejo, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori, aliyekuwa akipita magari mengine bila kuchukua tahadhari zinazohitajika, hali iliyosababisha kugonga gari dogo na kupoteza uelekeo.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewataka madereva kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, kufuata alama za barabarani na kuwa makini wanapotumia barabara ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha vifo na majeruhi.
...ends...



إرسال تعليق