Ad
Breaking🔥

HUKUMU YA LISU YAKWAMISHA MAZISHI YA KAKA YAKE WAKILI ALUTE MUGHWAI

FAMILIA YA LISSU YAHAIRISHA MAZISHI YA ALUTE KUSUBIRI HUKUMU YA TUNDU LISSU

Na Joseph Ngilisho-ARUSHA

FAMILIA ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, imesema mazishi ya kaka yao, Alute Mughwai Lissu, yatafanyika baada ya kupita kwa hukumu ya kesi inayomkabili Tundu Lissu, inayotarajiwa kutolewa Ijumaa, Novemba 6, mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Vincent Mughwai, ambaye ni msemaji wa familia na mdogo wa marehemu Alute, amesema familia imeamua kusubiri hukumu hiyo ili ndugu na jamaa waweze kushiriki katika shughuli hiyo ya kisheria jijini Dar es Salaam kabla ya kuendelea na taratibu za mazishi.

Marehemu Alute Mughwai Lissu amefariki dunia jana usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu. Katika siku za hivi karibuni alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian, Arusha, ambako hali yake ilizidi kuwa mbaya kabla ya mauti kumkuta.

Vincent amesema marehemu alikuwa mtu muhimu katika familia na ukoo, akitekeleza majukumu ya msemaji na kiongozi wa familia kwa ujumla.

Amesema mazishi yanatarajiwa kufanyika mkoani Singida, huku familia ikitarajia kutoa taarifa zaidi kuhusu tarehe na ratiba ya mazishi baada ya kukamilika kwa shughuli zinazohusiana na hukumu ya Tundu Lissu.


Ends

Post a Comment

Previous Post Next Post