Ad
Breaking🔥

DC LUGANGIRA AFIKISHA RAMBIRAMBI ZA RAIS SAMIA KWA FAMILIA ZILIZOPOTEZA WATOTO AJALINI

DC LUGANGIRA AFIKISHA RAMBIRAMBI ZA RAIS SAMIA KWA FAMILIA ZILIZOPOTEZA WATOTO AJALINI

Na Joseph Ngilisho | Arumeru

MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, amefikisha salamu za pole na rambirambi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa familia zilizopoteza watoto wao watatu katika ajali ya lori iliyotokea eneo la Ngaramtoni, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.

Lugangira amezifikia familia hizo kufuatia kifo cha wanafunzi watatu wa Kidato cha Tatu wa Shule ya Sekondari Mringa, waliofariki dunia baada ya kugongwa na lori katika Barabara ya Bypass, eneo la Kibaoni, Ngaramtoni, walipokuwa wakitoka shuleni.

 Mkuu huyo wa Wilaya aliwasilisha salamu za pole za Rais Samia kwa wafiwa, akiwapa pole kutokana na msiba huo uliogusa familia, shule na jamii kwa ujumla.

Watoto waliofariki katika ajali hiyo ni Jesca Sabore Ngotyek, Bianca Juma Mgongo na Catherine Pius Musa, ambao vifo vyao vimeacha simanzi kwa familia zao pamoja na wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari Mringa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, wanafunzi hao wanatarajiwa kuagwa Jumatatu, Novemba 2, 2026, katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mringa.






Post a Comment

Previous Post Next Post