DC LUGANGIRA AWATAKA DIASPORA,WATANZANIA WALIO NJE KUJISAJILI HAPA KWA MAENDELEO ARUMERU IJAYO KIMATAIFA
Na Joseph Ngilisho | ARUMERU
MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, amewaalika Watanzania wanaoishi ndani na nje ya nchi, hususan wenye asili ya Arumeru, kujisajili kupitia mpango wa Arumeru Diaspora kwa lengo la kushirikiana katika kuleta maendeleo ya wilaya hiyo.
Lugangira amewataka wenye nia ya kuchangia maendeleo ya Arumeru kupitia mawazo, utaalamu, uwekezaji na misaada kujaza dodoso lililotolewa, akieleza kuwa kila mmoja ana mchango muhimu katika maendeleo ya eneo hilo.
Amewataka wananchi kuscan QR Code iliyo kwenye tangazo hilo ili kupata fomu ya kujisajili na kujaza dodoso, huku akieleza kuwa mwisho wa kujaza ni Oktoba 21, 2026.
Amesema baada ya kujaza dodoso hilo, kutakuwa na taarifa na ratiba nyingine za ushirikiano zitakazotolewa kwa ajili ya kuimarisha ushiriki wa Watanzania hao katika maendeleo ya Arumeru.
Ends..



إرسال تعليق