MUME AMUUA MKE KISHA KWENDA KUNYWA POMBE NA KURUDI KUFANYA NAYE NGONO AKIWA MFU USIKU KUCHA
Na Joseph Ngilisho | DODOMA
MWANAMKE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa kwa kitu chenye ncha kali shingoni na mume wake, katika tukio linalodaiwa kuhusishwa na wivu wa kimapenzi lililotokea Mtaa wa Maili Mbili jijini Dodoma.Shemeji wa marehemu, Mohamed Iddy, amesema tukio hilo limetokea usiku na kwamba mtuhumiwa aliondoka nyumbani asubuhi na kuelekea kituo cha polisi, ingawa maelezo zaidi kuhusu mazingira ya tukio hilo bado yanatarajiwa kuthibitishwa na vyombo vya uchunguzi.
Baadhi ya majirani wa eneo hilo wameeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa akidaiwa kuwa na tabia ya kumpiga mke wake mara kwa mara kabla ya tukio hilo la kifo.
Wakizungumzia tukio hilo, majirani hao wameiomba Serikali kuhakikisha uchunguzi unafanyika kwa kina na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria, iwapo atabainika kuhusika na kifo hicho.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Maili Mbili, Maximilian Jeremiah, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa za awali zinaashiria kuwa huenda lilichochewa na wivu wa kimapenzi.
Jeremiah amesema mtuhumiwa tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi na hatua nyingine za kisheria.
Hata hivyo, mazingira kamili ya tukio hilo, chanzo cha ugomvi unaodaiwa kutangulia kifo hicho na maelezo rasmi kuhusu kilichotokea yanaendelea kusubiriwa kutoka kwa vyombo vya uchunguzi.
Kituo hiki kinaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ili kupata taarifa zaidi kuhusu tukio hilo, hatua zilizochukuliwa na maendeleo ya uchunguzi.
Ends


Post a Comment