Ad
Breaking🔥

ALIYEMUUA MKE NA BAADAYE KUFANYA NAYE NGONO AKIWA MFU,BABA WA MAREHEMU AMDAI MUUAJI MAHARI YA MILIONI 1.5 NDIPO WAKAZIKE

BABA WA MAREHEMU SHUKRANI ADAI MILIONI 1.5 ZA MAHARI KABLA YA MAZISHI

Na Arushadigital | DODOMA

BABA wa marehemu Shukrani Amos pichani kushoto, aliyeuawa kwa kudaiwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni jijini Dodoma, amedai Sh1.5 milioni kutoka kwa mume wa zamani wa binti yake, akieleza kuwa ni sehemu ya mahari ambayo haikukamilishwa katika ndoa yao ya awali.

Tukio la kifo cha Shukrani liliripotiwa Oktoba 9, 2026, katika Mtaa wa Mkwajuni jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, ambako mwili wa marehemu umehifadhiwa, baba huyo, Amos John, amesema binti yake aliolewa kwa mara ya kwanza na mwanaume mmoja na kufanikiwa kupata watoto wawili kabla ya ndoa hiyo kuvunjika.

Amesema baada ya kuachana na mume wake wa kwanza, marehemu aliolewa na mwanaume mwingine, ambaye walipata mtoto mmoja kabla ya uhusiano wao kuvunjika.

Baadaye, Shukrani aliolewa tena na mwanaume mwingine ambaye anadaiwa kuhusika na kifo chake.

Amos amesema madai yake ya Sh1.5 milioni yanatokana na mahari ambayo, kwa mujibu wake, haikukamilishwa katika ndoa ya kwanza ya binti yake.

Ameeleza kuwa anataka suala hilo la mahari litatuliwe kabla ya kuchukua mwili wa binti yake kwa ajili ya mazishi, akisema endapo suluhu haitapatikana, atazika mwenyewe.

Hata hivyo, maelezo kuhusu upande wa mwanaume anayedaiwa deni la mahari na hatua zinazoweza kuchukuliwa kutatua mgogoro huo hayakubainishwa katika taarifa hiyo.

Ends

Post a Comment

Previous Post Next Post