Breaking🔥

MWANAMKE AMUUA MUMEWE KWA KUMNYIMA UNYUMBA MOROGORO

MWANAMKE ADAIWA KUMUUA MUMEWE KWA KUMNYIMA UNYUMBA MOROGORO

Na Arushadigital|MOROGORO 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia mwanamke mwenye umri wa miaka 30, Jovita Bategeye Budyo, fundi cherehani na mkazi wa Mafisa, kwa tuhuma za kumuua mumewe, Abeli Charles (44), mfanyabiashara na mkazi wa eneo hilo.

Tukio hilo limetokea usiku wa Agosti 31, 2026, katika Mtaa wa Mafisa kwa Mambi, Kata ya Mafisa, Wilaya ya Morogoro Mjini, ambako mtuhumiwa na marehemu walikuwa wakiishi pamoja.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, kabla ya tukio hilo kutokea, wawili hao waligombana baada ya mtuhumiwa kudaiwa kumkatalia marehemu kufanya naye tendo la ndoa.

Inadaiwa kuwa wakati wa ugomvi huo, Jovita alichukua kitu chenye ncha kali na kumkata Abeli katika maeneo ya shingoni na kichwani, hatua iliyomsababishia majeraha makubwa.

Marehemu alijeruhiwa vibaya na baadaye alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.

Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Jovita, ambaye anaendelea kushikiliwa kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Kantimbo ametoa wito kwa wananchi kuepuka kutumia nguvu wakati wa migogoro ya kifamilia na badala yake kutumia njia za mazungumzo au kuwashirikisha viongozi na vyombo husika katika kutatua tofauti zao.

Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Ends..

Post a Comment

أحدث أقدم