Breaking🔥

MKUU WA MKOA ATONGOZWA NA SOPHIA,AAGIZA AKAMATWE

MKUU WA MKOA ATONGOZWA NA SOPHIA

Na Joseph Ngilisho |Arushadigital /TABORA

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha, amesimulia kisa cha mwanadada aliyemtaja kwa jina la Sophia, aliyekuwa akimtumia ujumbe mfupi wa simu wa kumtongoza licha ya kuonywa mara kadhaa kuacha tabia hiyo.

Chacha amesema Sophia aliendelea kumtumia ujumbe huo mara kwa mara, jambo lililomlazimu kuchukua hatua kwa kulifikisha suala hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC), hatua ambayo imeelezwa kuwa ilifanikiwa kumfanya mwanadada huyo kusitisha kabisa ujumbe huo.

Akisimulia kisa hicho, Chacha amesema kabla ya kufikia hatua ya kulifikisha suala hilo kwa RPC, alijaribu kutumia njia mbalimbali kumfikia Sophia, ikiwemo kutuma wajumbe waliokwenda kumuonya na kumtaka kuacha kumtumia ujumbe wa aina hiyo.

Hata hivyo, amesema juhudi hizo hazikuzaa matunda, kwani Sophia aliendelea na msimamo wake wa kumtumia ujumbe, hali iliyosababisha suala hilo kuchukuliwa hatua zaidi.

Chacha amesimulia kisa hicho Septemba 7, 2026, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi iliyofanyika baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha uongozi wa Mkoa wa Tabora.

Katika hafla hiyo, Chacha alikabidhi rasmi majukumu ya uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa Mkuu wa Mkoa mpya, Beno Malisa, katika hatua ya kuanza kwa uongozi mpya wa mkoa huo.

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم