Breaking🔥

LISU AIGARAGAZA JAMHURI ,IGP, MKUU WA MAJESHI NA MKUU WA UPELELEZI KUITWA MAHAKAMANI

MAHAKAMA YAWAITA WAKUU WA USALAMA KATIKA KESI YA LISSU

By Arushadigital-Dar Es Ealaam



MAHAKAMA Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imewaita Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Ramadhani Kingai, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillus Wambura na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Jacob Mkunda, kufika mahakamani.

Wito huo umetolewa wiki chache baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini, kuwataja viongozi hao miongoni mwa watu anaowahitaji kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Lissu, kupitia upande wake wa utetezi, aliwasilisha ombi la kutaka baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kuitwa mahakamani ili kutoa ushahidi unaohusiana na masuala yanayojadiliwa katika kesi hiyo.

Mbali na Kingai, Wambura na Jenerali Mkunda, Lissu aliwataja pia Rais Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwa miongoni mwa watu anaowahitaji kama mashahidi wake.

Kesi hiyo imeendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu huku upande wa utetezi ukiendelea kuwasilisha mashahidi wake, katika hatua muhimu ya kesi hiyo ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti huyo wa Chadema.

Ends

Post a Comment

أحدث أقدم