Breaking🔥

HAFIDH AMEIR, MUME WA RAIS SAMIA, AFARIKI DUNIA

HAFIDH AMEIR, MUME WA RAIS SAMIA, AFARIKI

Na Joseph Ngilisho | Arushadigital

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Deogratius Ndejembi, ametangaza kifo cha Mhe. Hafidh Ameir Hassan, mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Hafidh Ameir amefariki dunia leo, Jumatatu, Septemba 7, 2026, majira ya asubuhi.

Kifo hicho kimekuja ikiwa ni msiba mkubwa kwa Rais Samia, familia, ndugu, jamaa na Watanzania kwa ujumla.

Taarifa rasmi ya Ikulu inaeleza kuwa Rais Samia amekuwa katika ndoa na Hafidh Ameir na wamejaliwa watoto wanne.

Hafidh Ameir amekuwa akijulikana zaidi kwa nafasi yake kama mwenza wa Rais Samia, huku familia yao ikiwa sehemu ya maisha ya Rais tangu kabla ya kushika nafasi za juu za uongozi nchini.

Tangazo la kifo hicho linatarajiwa kufuatiwa na taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi, ratiba ya kuuaga mwili na namna taifa litakavyoshiriki katika kuomboleza msiba huo.


Ends...

Post a Comment

أحدث أقدم