TRA ARUSHA YAVUKA LENGO, YAKUSANYA SH520 BILIONI
Na Joseph Ngilisho | ARUSHA
Shuma alisema ongezeko hilo ni sawa na zaidi ya Sh25 bilioni, akieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano kati ya TRA, walipa kodi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali.
Akizungumza leo Agosti 29,2026 katika hafla ya kuwapongeza walipa kodi na wadau wa TRA mkoani Arusha, Shuma alisema utayari wa wafanyabiashara kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi, sambamba na huduma bora zinazotolewa na watumishi wa TRA, umechangia kwa kiasi kikubwa kufikia mafanikio hayo.
“Mafanikio haya yasingewezekana bila ushirikiano na utayari wa walipa kodi kulipa kodi, pamoja na watumishi wa TRA kutoa huduma bora kwa walipa kodi na wadau wanaofika kupata huduma,” alisema.
Shuma alisema TRA Arusha pia imeanza mwaka wa fedha 2026/2027 kwa kasi, baada ya mwezi Julai kukusanya Sh49.82 bilioni dhidi ya lengo la Sh42.69 bilioni.
Alisema makusanyo hayo ni ziada ya Sh7.2 bilioni, sawa na ufanisi wa asilimia 116.
“Tumeweza kuanza vyema na tunaendelea kutoa shukrani kwa walipa kodi na watumishi wote ambao wamefanya kazi kwa bidii, uelewa, uaminifu na uadilifu mkubwa,” alisema.
SHUMA AWAPONGEZA WADAU
Aidha, Shuma aliwapongeza wafanyabiashara na wadau mbalimbali kwa ushirikiano wanaoupa TRA katika kuongeza makusanyo ya Serikali.
Alivitaja vyama vya wafanyabiashara na wadau wa sekta ya utalii ikiwamo TATO, TLTO, TTGA na TAUTO, pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania na AKIBOA.
Alisema ushirikiano huo umekuwa muhimu katika kujenga uelewa kuhusu ulipaji kodi na kuhakikisha wafanyabiashara wanatimiza wajibu wao kwa Serikali.
Shuma pia aliwatambua watumishi wa TRA kuwa sehemu muhimu ya mafanikio hayo, akisema bidii, uaminifu na uadilifu wao katika kuwahudumia walipa kodi umechangia kuimarisha makusanyo.
Alisema TRA itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wafanyabiashara na wadau wengine ili kuimarisha ulipaji kodi, kuboresha huduma na kuongeza mapato ya Serikali.
Ends








إرسال تعليق