FLYING HORSE OILS YAINGIA ARUSHA KWA KISHINDO, YALETA MAPINDUZI YA MAFUTA YA INJINI KASKAZINI

FLYING HORSE OILS YAINGIA ARUSHA KWA KISHINDO, YALETA MAPINDUZI YA MAFUTA YA INJINI KASKAZINI

...Yafungua ofisi ya kwanza Arusha, yaahidi mafuta yanayodumu hadi kilomita 20,000; kampuni kubwa za usafiri zatangaza kuendelea kuyaamini

Na Joseph Ngilisho | ARUSHA

KAMPUNI ya ALC Lubricant inayozalisha na kusambaza vilainishi vya chapa ya Flying horse Oils imezindua rasmi ofisi yake ya kwanza katika jiji la Arusha, hatua inayotajwa kufungua ukurasa mpya wa biashara ya mafuta ya vilainishi (lubricants) katika Kanda ya Kaskazini kwa kusogeza huduma karibu na wateja na kuongeza upatikanaji wa bidhaa zenye viwango vya kimataifa.

Uwekezaji huo unatarajiwa kuwanufaisha maelfu ya wamiliki wa magari binafsi, mabasi, malori, pikipiki, bajaji, mitambo ya ujenzi, migodi na viwanda ambao kwa muda mrefu walilazimika kutegemea bidhaa kutoka maeneo ya mbali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa Flying horse Oils,leo Jumatatu Julai 27,2026 Afisa masoko wa kanpuni hiyo ,Abdulrahman Baharia, alisema kampuni imechagua Arusha kutokana na kukua kwa shughuli za uchumi katika ukanda wa kaskazini na mahitaji makubwa ya mafuta bora ya vilainishi.

Alisema dhamira ya kampuni ni kuwapatia wateja bidhaa halisi zinazolinda injini, kuongeza ufanisi wa vyombo vya moto na kupunguza gharama za matengenezo.

"Mafuta ya injini ni uhai wa gari. Ukichagua mafuta bora unaongeza maisha ya injini, unapunguza gharama za matengenezo na unapata matumizi yenye tija zaidi," alisema Baharia.

Alieleza kuwa baadhi ya mafuta yanayozalishwa na kampuni ya ALC Lubricant kupitia chapa ya Flying horse Oils yana uwezo wa kutumika hadi kilomita 10,000 na mengine kufikia 20,000, kutegemeana na aina ya gari na maelekezo ya mtengenezaji.

Baharia alisema kampuni hiyo tayari imejijengea soko kupitia taasisi za serikali, kampuni za usafiri na waendeshaji wa mitambo mizito, huku ofisi ya Arusha ikiwa ya 10 nchini baada ya Dar es Salaam, Mwanza, Geita, Mbeya, Moshi na maeneo mengine.

Aliwahimiza wananchi kununua mafuta kutoka kwa mawakala wanaotambulika ili kujiepusha na bidhaa bandia zinazoweza kuharibu injini.

Katika uzinduzi huo, mmoja wa wadau wakubwa wa kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya , Masalu  Class, alitangaza kuendelea kutumia bidhaa za Flying horse Oils kutoka kampuni ya kutokana na ubora wake.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo, Meneja wa Uendeshaji, Domisiani Rwezahura, alisema matumizi ya mafuta hayo yamechangia kuboresha utendaji wa mabasi yao na kupunguza gharama za matengenezo.

"Tumekuwa tukitumia bidhaa hizi kwa muda mrefu na tumeona matokeo yake. Zinailinda injini, zinaongeza ufanisi wa magari na zinapunguza gharama za uendeshaji. Tunawahamasisha wamiliki wa magari, mabasi, bodaboda na bajaji kutumia mafuta yenye ubora kama haya," alisema.

Kwa kufungua ofisi Arusha, Flying horse Oils inalenga kuifanya Kanda ya Kaskazini kuwa kitovu kipya cha usambazaji wa bidhaa zake, huku ikiahidi huduma za haraka, upatikanaji wa bidhaa wakati wote na ushirikiano wa karibu na wafanyabiashara wa ndani ili kuimarisha sekta ya usafiri, biashara na viwanda.

Ends

Post a Comment

Previous Post Next Post