BINTI AMUUA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA KUZUIWA KWENDA KWENYE BARTHDAY


BINTI AMUUA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA KUZUIWA KWENDA KWENYE BARTHDAY

Na Joseph Ngilisho

PWANI – Msichana mwenye umri wa miaka 16 anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi, baada ya kudaiwa kuzuiwa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake katika Kijiji cha Msoga, Wilaya ya Chalinze.

Mtuhumiwa, aliyefahamika kwa jina la Rahma Musa Tito, anadaiwa kumuua mama yake, Hadija Hemedi Shaha (51), aliyekuwa mkulima na mwenye ulemavu wa miguu yote miwili.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, tukio hilo lilitokea usiku wa Julai 28, 2026, majira ya saa 5:00 usiku, baada ya marehemu kumzuia binti yake kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake iliyokuwa ikifanyika karibu na Hospitali ya Msoga.

Polisi wamedai kuwa baada ya kuzuiwa, Rahma alianza kumshambulia mama yake kabla ya kumchoma kichwani kwa kutumia kitu chenye ncha kali, na kusababisha majeraha yaliyodaiwa kupelekea kifo chake.

Tukio hilo lilibainika asubuhi ya Julai 29, 2026, baada ya fundi ujenzi aliyekuwa akidai malipo na kufuata mfuko wa saruji kufika nyumbani kwa marehemu. Baada ya kugonga mlango, alifunguliwa na mtuhumiwa, ndipo alipouona mwili wa Hadija ukiwa umelala sakafuni ukiwa na majeraha makubwa kichwani yaliyokuwa yakivuja damu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limesema Rahma anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini mazingira yote ya tukio hilo kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.

...Ends....

Post a Comment

Previous Post Next Post