ILO YAZINDUA MWONGOZO WA HABARI ZA UHAMAJI; JOWUTA YATIA NENO
By Arushadigital, Mombasa
Mwongozo huo umezinduliwa jana Ijumaa, Juni 20,2026 na Mshauri Mkuu wa Kiufundi kutoka ILO, Charles Autheman katika warsha ya viongozi wa
Vyama vya Wafanyakazi vya Wanahabari katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki inayoendelea Mombasa nchini Kenya.
Akizindua mwongozo huo, Autheman amesema sasa unapatikana katika mtandao wa ILO ukiwa katika lugha ya Kingereza, Kifaransa, Kiarabu na nyinginezo isipokuwa Kiswahili.
Mtaalam huyo amesema bado kuna changamoto katika uandishi wa habari za wahamaji na wakimbizi hivyo ILO imetoa mwongozo huo ili kurahisisha uandishi ikiwamo matumizi ya maneno yasiyo na ukakasi.
"Tunalifanyia kazi lakini pia Tanzania mnaweza kutafsiri mwongozo huu kwa lugha ya Kiswahili," amesema mtaam huyo akijibu hoja hiyo.
Warsha hiyo imeandaliwa na ILO kwa kushirikiana na Shirikisho la Wanahabari Afrika (FAJ), Shirikisho la Wanahabari Afrika Mashariki (FEAJ) na Chama cha Waandishi nchini Kenya (KUJ) .
Warsha hii ya kikanda imehudhuriwa na viongozi wa vyama na mashirika ya wanahabari kutoka Comoro, Jibuti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.





إرسال تعليق