DIDIER DROGBA AVUTIA WABUNGE BUNGENI, LUKUMAY ANG’ARA KATIKA SALAMU
By Arushadigil|DODOMA
Nyota wa zamani wa soka duniani, Didier Drogba, amezua gumzo bungeni baada ya kuwasili katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jijini Dodoma, ambapo wabunge wengi walijitokeza kwa wingi kugombea nafasi ya kumsalimia.
Miongoni mwa wabunge waliofanikiwa kupata nafasi hiyo ni Johannes Lembulung Lukumay, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, ambaye alionekana kung’ara miongoni mwa wabunge kwa kupata fursa ya kusalimiana na nyota huyo maarufu kutoka Ivory Coast.
Tukio hilo lililofanyika leo Mei 4, 2026, limevutia hisia za wengi ndani na nje ya ukumbi wa Bunge, likionesha namna ambavyo ujio wa Drogba ulivyokuwa na mvuto mkubwa kwa viongozi na wadau mbalimbali.
Drogba, ambaye aliwahi kutamba katika vilabu vikubwa duniani, ameendelea kuwa nembo ya mafanikio katika soka la Afrika, hali iliyochangia mapokezi makubwa aliyopata alipowasili nchini.
Ends..

0 Comments