MTOTO WA MWISHO WA RAIS MUGABE MBARONI AFRIKA KUSINI AKIJARIBU KUUWA

 MTOTO WA MWISHO WA Robert Mugabe AKAMATWA AFRIKA KUSINI AKIKABILIWA NA TUHUMA YA KUJARIBU KUUWA

Na ArushaDigital – Afrika Kusini


Polisi nchini Afrika Kusini wamemkamata Bellarmine Mugabe (28), mtoto wa mwisho wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, kufuatia tukio la ufyatuaji risasi lililoripotiwa katika nyumba ya makazi iliyopo eneo la kifahari la Hyde Park jijini Johannesburg.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, mwanaume mwenye umri wa miaka 23—anayesadikiwa kuwa mtunza bustani katika makazi hayo—alipigwa risasi na kujeruhiwa. Hali ya majeruhi haikuelezwa mara moja na mamlaka.

Maafisa wa usalama waliofanya upekuzi katika nyumba aliyokuwa akiishi Bellarmine walipata risasi, hata hivyo hakuna silaha iliyokutwa eneo la tukio.

Bellarmine Mugabe ni mtoto wa mwisho wa marehemu Robert Mugabe na mkewe wa pili, Grace Mugabe. Hayati Mugabe aliiongoza Zimbabwe kwa zaidi ya miongo mitatu kabla ya kuondoka madarakani mwaka 2017, na alifariki dunia mwaka 2019.

Polisi pia wamemkamata mtu mwingine kuhusiana na tukio hilo, huku uchunguzi ukiendelea kubaini mazingira kamili ya tukio. Msemaji wa polisi, Kanali Dimakatso Nevhuhulwi, amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kuahidi taarifa zaidi zitatolewa uchunguzi utakapokamilika.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments