MADURO APANDISHWA KIZIMBANI CHINI YA ULINZI MZITO

Rais wa Zamani wa Venezuela Nicolás Maduro Afikishwa Mahakamani Marekani Baada ya Kukamatwa

By Arushadigital 

New York, Marekani – Rais wa zamani wa Venezuela, Nicolás Maduro, ambaye aliondolewa madarakani, amefikishwa leo katika mahakama ya Manhattan, New York, Marekani, baada ya kukamatwa katika operesheni maalum ya Marekani. Orodha kamili ya mashtaka dhidi yake imepangwa kusomwa leo.

Maduro anatuhumiwa na serikali ya Marekani kwa biashara haramu ya dawa za kulevya, makosa yanayohusiana na silaha, na kuendesha utawala wa kigaidi wa dawa za kulevya, madai ambayo kiongozi huyo amayaikana.

Pia, mkewe wa Maduro, Cilia Flores, alikamatwa katika operesheni hiyo na anatuhumiwa kwa rushwa, hatua inayozidisha shinikizo la kisheria kwa familia ya kiongozi huyo wa zamani.

Hali hii imesababisha mvutano wa kimataifa, huku washirika wa Maduro, ikiwemo China na Iran, wakiiita Marekani ichukue hatua ya kumwachilia huru. Serikali ya Beijing imekosoa operesheni hii, ikisema kuwa vitendo vya Washington ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.




Chanzo: BBC


Post a Comment

0 Comments