By arushadigtal
Rais wa muda mrefu wa Uganda, Yoweri Museveni (80), ametangazwa kuwa Mgombea atakayekiwakilisha Chama tawala katika Uchaguzi wa Rais mwaka ujao, na kumfungulia njia ya kutaka kuongeza takriban miaka 40 madarakani.
Katika hotuba yake, Museveni alisema kuwa ameitikia wito huo na ikiwa atachaguliwa, ataendelea na dhamira yake ya kuigeuza Uganda kuwa nchi ya kipato cha kati.
Wakosoaji wa Museveni wanasema ametawala kwa mkono wa chuma tangu alipotwaa Mamlaka kama Kiongozi wa waasi mwaka 1986.
Ameshinda kila uchaguzi uliofanyika tangu wakati huo na katiba imefanyiwa marekebisho mara mbili ili kuondoa ukomo wa umri na muda ili kumruhusu kusalia Madarakani.
Mwanamuziki nyota wa Pop, Bobi Wine anatarajiwa kuwa Mpinzani Mkuu wa Museveni katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Januari ijayo.
0 Comments