KIJANA MDOGO MWENYE PESA NYINGI NATHAN KIMARO ATIKISA KANISA LA KKKT OLORIENI,AMWAGA MAMILIONI A to Z YAMSAPOTI VITI KIBAO,AMPIGIA SIMU MAKONDA NA WAZIRI SLAA NAO WACHANGIA

Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 


MFANYABIASHARA, Nathan Kimaro amewaasa vijana kuepuka kukaa kwenye vikundi vinavyohalalisha  umaskini ikiwemo vijiwe vya Boda boda badala yake watumie mitandao ya kidigitali na kusoma magazeti ili kubaini fursa za kiuchumi kwa ajili ya kujiletea maendeleo.


Kimaro ambaye ni kijana mdogo mwenye pesa nyingi ,ameyasema hayo leo juni 6,2025 wakati akizungumza na vijana kama mgeni mwalikwa  katika ibada ya jumapili katika kanisa la KKKT dayosisi ya Kaskasini Kati, usharika wa Olorieni jijini Arusha,iliyoambatana na harambee ya kuchangia maendeleo ya vijana na ujenzi wa kanisa hilo.


"Vijana waepuke vikundi vinavyohalalisha umaskini ikiwemo vijiwe vya waendesha pikipiki,wajitume ,wasome magazeti kuna fursa nyingi za kibiashara na kilimo watajua hata bei za mazao"

Alisema kuwa vijana wananafasi kubwa ya kufikia mafanikio iwapo watakubali kujiendeleza ikiwemo kusoma majarida ili kupata fursa mbalimbali za kibiashara.


Aidha aliwasihi wazazi kuacha kuwabeza watoto wao wanapotafuta mafanikio jambo  linalowatia woga na hofu ,badala yake wawatie moyo na kuwaunga mkono ili kutimiza ndoto zao.



Akiongea kwa njia ya Simu baada ya kupigiwa kanisani hapo, waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Jerry Slaa aliwaasa vijana kutumia muda wao mwingi kujiendeleza kwa kutumia mitandao ya kidigitali na kusoma magazeti ili kubaini fursa za kiuchumi.


Alitolea mfano wa Kijana Mfanyabiashara ,Natan Kimaro ambaye amefanikiwa akiwa na umri mdogo ikiwa ni jitihada zake zilizotokana na kujituma  .


"Msingi mkubwa wa mafanikio kwa kijana ninkujotuma kupenda kusoma na kujiingiza katika makundi yasiyo na dira ya maendeleo "


Slaa alichangia kiasi cha sh,milioni mbili kwa ajili ya maendeleo ya vijana wa kanisa hilo zitakazowasaidia kuanzisha mradi wa  kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Paulo Makonda akiongea kwa njia ya simu alimshukuru Mfanyabiashara Kimaro kwa kumkutanisha na waumini wa kanisa hilo na kuwaomba waendelee kuliombea Taifa,Rais wetu Samia Suluhu Hasani pamoja na  kujiombea wao wenyewe na nafsi zao.


Alisema akiwa  sehemu ya waumini wa kanisa atashiriki ujenzi wa kanisa hilo kwa kuchangia kiasi cha sh, milioni tano na pia aliahidi kutoa sh,milioni moja kwa ajili ya mradi wa maendeleo ya vijana wa kanisa hilo.


Katika ibada hiyo Kimaro aliwezesha kupatikana kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 20 kutoka kwa rafiki zake kwa ajili ya ujenzi wa kanisa na maendeleo ya vijana huku yeye akichangia viti  vilivyotolewa na kiwanda cha Nguo cha A To Z kwa ajili ya mradi wa vijana wa kanisa hilo.


Pia Kimaro alitoa sh,milioni 3 tasilimu na kuahidi kutoa sh, Laki tano kwa ajili ya usafi wa kanisa hilo. 

Wengine waliochangia ni Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda ambaye alichangia sh,milioni 2.













Ends....









Post a Comment

0 Comments