By arushadigtal-DODOMA
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeahirisha Kikao, kilichotakiwa kufanyika leo julai 19,2025 cha Kuchuja Wagombea wa Ubunge kupitia Chama hicho, Mchujo huo utafanyika tarehe 28 Julai, 2025 .
"Hakuna mtu aliyekatwa, hakuna mtu aliyefyekwa kama ilivyoandikwa. Kwa hiyo, mpaka tarehe 28 ndiyo itakuwa taarifa ya mwisho wa uteuzi wa wagombea, hivyo wananchi watulie." - Amos Makalla, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amos Makalla amesema sababu kubwa ya vikao vya Uteuzi wa wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani kusogezwa mbele ni kutokana na wingi wa wagombea ambapo kwa nafasi za Udiwani ni zaidi ya elfu 27 na Ubunge ni zaidi ya elfu 10
Makala amesema mchakato wa wagombea hao sasa ni Julai 28 huku akisema kuwa ratiba kwa nafasi za wagombea wa viti maalum wa madiwani tarehe zake hazijabadilika ni ile Julai 22
"Mchakato ndani ya Chama unaendelea vizuri na kufanyika Julai 28 badala ya leo Julai 19," CPA Amos Makalla. #EastAfricaTV
Wakati CCM ikiahirisha kwa muda mkeka wa wagombea uliokuwa utoke leo,zipo taarifa kwamba baadhi ya watia nia hawalali,kila siku wapo Dodoma kujaribu kuweka sawa majina yao yaweze kurudi majimboni.
Watia nia hao wanahofu kutorejea kwa majina yao na wengine waliokatwa ngazi ya wilaya na Mkoa wanajaribu kuwashawishi wajumbe kwa namna yoyote ile ili majina yao yaweze kurejeshwa.
0 Comments