WANANCHI MAKUYUNI WAFURIKA MAHAKAMANI ,MWENZAO AKISHTAKIWA NA MTENDAJI WA KATA,MSHTAKIWA AMKATAA HAKIMU ASEMA ANAUSWAHIBA NA WALALAMIKAJI,HAKIMU AGOMA KUJITOA

 Joseph Ngilisho MONDULI

Wananchi wa kata ya Makuyuni Monduli Mkoa wa Arusha,wamelazimika kufurika katika mahakama ya Mwanzo ya Mto wa Mbu,Monduli kufuatia mwananchi mwenzao John Laisangai kushtakiwa na Mtendaji wa kata hiyo Grace Mayunga wakidai ni kesi ya kupika inayolenga kufifisha jitihada zao za kupambana na viongozi wanaohujumu  maeneo katika kata yao.


John Laisangai mkazi wa Makuyuni ameshtakiwa kwa kosa la kutishia kwa mwandishi kupitia barua inayodaiwa kuiandika kwenda kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha 

Katika shauri hilo namba 234/2023 Laisangai anatuhumiwa kutenda kosa hilo Agosti 1 mwaka huu kwa kuandika barua hiyo kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ikimtaka kumchukulia hatua mtendaji huyo kutokana na  matumizi mabaya ya ofisi huku barua hiyo ikisisitiza kuwa 'vinginevyo watajichukulia sheria mkononi'.


Mbele ya Hakimu Mary Mganga kesi hiyo ilikuja kwa hatua za kusikilizwa na shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji Grace Mayunga alitoa ushahidi wake hata hivyo alishidwa kukamikisha ushahidi wake mara baada ya mshitakiwa kuhoji ilipo barua inayodaiwa aliandika.


"Mheshimiwa hakimu siwezi kuendelea kumhoji mlalamikaji na mashahidi wengine kwa sababu barua anayodai nimeandika na kumtishia kwa maneno ipo wapi'???


Hata hivyo mshtakiwa katika kesi hiyo  aliibua hoja ya kumkataa hakimu kwa madai kwamba hana imani na kutoa  sababu kuwa alimnyima dhamana siku anasomewa shitaka mahakamani wakati ni haki ya mshtakiwa


Hoja nyingine Laisangai alimtuhumu hakimu huyo kuhusika katika uuzwaji wa maeneo ya kijiji kwa kutumia mhuri wake kama shahidi jambo ambalo alidai kuwa anashirikiana na upande wa walalamikaji ambao ndio wanahusika na uuzaji wa maeneo ya kijiji hicho.


Baada ya hoja hizo hakimu aliahirisha shauri hilo kwa muda na aliporejea alitoa maamuzi ya kukataa  ombi la mshtakiwa kuhusu kujitoa akidai halina msingi baada ya hoja hizo kuonekana hazina mashiko.


"Sababu alizozitoa mshtakiwa hazina mashiko na mimi nimejipima na kuona hakuna sababu ya kujitoa na kesi iendelee"


Hata hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 3 mwaka huu baada ya mlalamikaji kushindwa kuwasilisha barua ya madai yake mahakamani, na hakimu alimtaka mlalamikaji kuleta barua hiyo  pamoja na kutoa onyo kwa mashahidi wake sita kufika mahakamani.




Ends....










Post a Comment

0 Comments