JESHI KUJENGA NYUMBA ZA BILIONI 97 MSOMERA,LASAINI MKATABA NA MAMLAKA YA NGORONGORO,LITATUMIA MIEZI SITA TU KUMALIZA NYUMBA 5000,WAMASAI SASA KUJENGEWA SELFU

 Na Joseph Ngilisho Arusha 

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)na Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kupitia shirika la SUMA -JKT zimesaini hati ya makubaliano ya sh,bilioni 97 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zipatazo 5000 katika eneo la Msomera kwa ajili ya makazi ya wananchi wanaohama kwa hiyari kutoka eneo la Hifadhi wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha.






Akiongea na vyombo vya habari Kamishna wa uhifadhi NCAA,Fred Manongi alisema ujenzi wa nyumba hizo unatekelezwa na SUMA JKT kwa gharama ya sh,bilioni 97 na unatarajiwa kuanza mapema Oktoba 1,mwaka huu na kukamilika ndani ya miezi sita.

Manongi alisema ujenzi wa nyumbani hizo ni mwendelezo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 503 na  kati ya hizo SUMA JKT ilijenga nyumba 403 na kufanikiwa kuhama kwa kaya 551 zenye watu 3,010 na mifugo 15,321.

Alisema tangu kuanza kwa zoezi hilo juni ,2022 makundi 19 yenye kaya zaidi ya 565  zenye watu 3097  na mifugo zaidi ya 15,500 na kwamba hadi sasa jumla ya kaya 1524 zimeshahama ndani ya hifadhi hiyo.

Aidha alisisitiza kuwa mamlaka ya Ngorongoro  imekuwa ikiwashirikisha kikamilifu wakazi hao wakati wa ujenzi wa nyumba katika eneo la Msomera ili kuepusha malalamiko na kuzingatia haki ya kuishi wao na familia zao.

"Kwa sasa tunajenga nyumba za vyumba vitatu kwa ajili ya familia hizo japo ni gharama kubwa lakini rais wetu ni kiongozi mwenye upendo na huruma kwa wanachi wake amesikia kilio  "alisema.

Kwa upande wake mkuu wa jeshi la kujenga Taifa JKT,Meja Jenerali Rajab Mabele alisema kuwa mradi wa ujenzi wa nyumba 5000 eneo la Msomera ni mradi wa pili kutekelezwa na jeshi hilo baada ya mradi wa kwanza wa nyumba 402 kukamilika kwa ufanisi mkubwa ndani ya miezi mitatu.

Meja Mabele alisema kuwa ndani ya miezi sita watakamilisha ujenzi wa nyumba hizo 5000 kwa kuwa nia ya kufanya kazi hiyo na sababu wanayo na uwezo wanao.

"Jukumu hili ambalo tumekabidhiwa jeshi la kujenga taifa ni miongoni mwa majukumu yetu matatu hili ni jukumu letu la kulinda watanzania tunashukuru kwa kuaniniwa"

Ends.. 










Post a Comment

0 Comments