Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mkurugenzi wa Tiba nchini,Prof Paschal Ruggajo kutoka wizara ya Afya amesema kuwa rais Samia Suluhu Hasan amewekeza kiasi cha sh, trilion 6.7 katika sekta ya afya kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake ili kuboresha miundo mbinu ya afya ,vifaa tiba na madawa.
Aidha amesema serikali imetenga sh,bilioni 4 kwa ajili ya kuiwezesha taasisi ya CEDHA ya mkoa wa Arusha kutoa mafunzo ya umahiri kwa viongozi wa afya wa ngazi mbalimbali katika hospitali za mikoa na rufaa nchini.
Aliagiza wakurugenzi wote wa hospitali za Taifa ,Kanda pamoja na waganga wafawidhi wa hospitali zote za mikoa na rufaa kuhakikisha wana kitumia kituo cha CEDHA katika kuendesha mafunzo mbalimbali ya afya ikiwemo utafiti na tiba.
Akiongea katika mafunzo yanayoendelea katika kituo hicho cha Cedha kilichopo jijini Arusha, Prof.Ruggajo alisema rais Samia amelenga kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya afya kwa kuelekeza huduma bora na wananchi kutotembea umbali wa zaidi ya kilometa tano kufuata huduma ya afya.
Alisema wizara ya Afya imeanza mkakati wa kukiwezesha kituo cha CEDHA kwa kukipatia rasilimali fedha kuhakikisha taasisi hiyo inasimama imara na kutoa huduma kama yalivyokuwa malengo ya mwasisi wa chuo hicho hayati Mwl.Julias Nyerere.
"Tumepewa majukumu ya kuhakikisha tunapata viongozi watakaotengeneza mtaala ambao utatumika kujenga uwezo kwa ajili ya viongozi wa sasa"
Awali Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba na MRATIBU WA TAFITI WA WIZARA YA AFYA
Luteni Kanali dkt Pius Gerald Horumpende Kabusubuto alisema mafunzo hayo yatatoa mwanga na kuwezesha viongozi kuwa na uongozi bora na utawala bora
"Mafunzo haya ni muhimu sana katika sekta ya afya hasa ukizingatia kwamba rais samia katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake ameweka uwekezaji mkubwa wa fedha"
Alisema katika mwaka wa fedha 2023/24 serikali imetenga sh bilioni nne kwa ajili ya kukiwezesha kituo cha CEDHA kutoa mafunzo hayo muhimu kwa uongozi bora katika kusimamia huduma za afya na hospitali za rufaa nchini pamoja na kuimarika tafiti za afya .
Naye mkuu wa Taasisi hiyo Dkt Johannes Lukumay,alisema kuwa taasisi ya CEDHA imejipanga vema kutoa mafunzo ya Uongozi na usimamizi wa huduma za afya kwa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza
Dkt Lukumay alimpongeza rais Samia kwa kuendelea kuwekeza fedha za kutosha katika sekta ya afya pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maendeleo nchini.
Ends..
.
0 Comments